NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
MKOA wa Pwani, umepata washukiwa wanne wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu,(COVID- 19) ,ambao tayari wamechukuliwa sampuli na majibu yameonyesha hawana ugonjwa huo ,hivyo hadi sasa mkoa huo upo salama.
Aidha serikali mkoani hapo ,imeiomba wizara ya afya kuona umuhimu wa kupeleka vifaa vinavyotumika kupima joto kwa wageni wanaoshuka katika kiwanja cha ndege cha Mafia ,ambacho kinapokea watalii na wageni kutoka nje ya nchi kama ilivyo uwanja wa ndege wa Mwl.Nyerere.
Akifungua kikao cha wajumbe wa kamati ya afya ya msingi kuhusu ugonjwa wa Corona ,mjini Kibaha, mkuu wa mkoa huo,mhandisi Evarist Ndikilo alieleza ugonjwa huo ni tishio , ukizingatia mkoa wa Pwani upo karibu na Dar es salaam na uwanja wa ndege wa kimataifa na unapokea watalii.
Alisema,wagonjwa wanne walioshukiwa kupitia timu za kudhibiti ugonjwa huo mkoa na halmashauri RRT walifika kwa haraka na kuchukuliwa sampuli ambapo majibu yalionyesha kuwa hawana corona.Aliwatoa hofu wananchi wa mkoa huo ,na kuwaomba kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huo kwa kufuata miongozo inayotolewa na idara ya afya na serikali.
Ndikilo,alizuia mikusanyiko isiyo ya lazima, mikutano,kusitisha shughuli za michezo na matamasha,makongamano na kutoa maelekezo ya fedha zilizopangwa kwa ajili ya Mwenge zitumike kupambana na ugonjwa wa COVID -19.
Nae mganga mkuu wa mkoa wa Pwani ,Dk.Gunini Kamba alisema lengo la kikao hicho ni kujadiliana namna ya kupambana na ugonjwa huo ,huku wakishirikishwa viongozi wa dini,madereva bodaboda na wafanyabiashara.
Gunini aliwaasa wananchi ,kufunika mdomo,na pua wakati wa kukohoa kwa kitambaa safi,kunaww mikono kwa maji tiririka na sabuni,kuepuka kusalimiana kwa mikono na kukumbatiana.
Kwa upande wake ,sheikh mkuu wa mkoa huo, Hamis Mtupa aliitaka jamii isimuache mungu,iweke ibada mbele wakati ikijikinga na janga hilo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika la afya ulimwenguni, inasema ugonjwa wa Corona umeanzia nchi ya China ,na hadi kufikia march 18 mwaka huu jumla ya wagonjwa 191,127 wamethibitika kuugua ugonjwa huo ambapo watu 7,807 wamefariki. Kwa takwimu za Tanzania ,wagonjwa sita wamegundulika kuugua ugonjwa huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...