Na  Said Mwishehe, Michuzi Globu ya Jamii

NGOME ya Wanawake ya Chama cha ACT Walendo imetangaza safu ya viongozi wake wa idara mbalimbali ndani ya ngome hiyo huku mkakati mkubwa ukiwa ni kuweka mkakati na mipango ambayo itasaidia kufanikisha Chama hicho kushika Dola katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Akizungumza leo Machi 30 mwaka 2020 jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Ngome hiyo ya Wanawake wa ACT Wazalendo Mkiwa Kimwanga mwenyekiti kwenye uchaguzi wa ndani ya Chama hicho uliofanyika siku za karibuni sasa wamekamilisha safu ya uongozi kwa kuteua wakuu wa idara mbalimbali za ngome hiyo.

Mkiwa Kimwanga amefafanua kwamba uteuzi huo ni Makatibu na Manaibu Katibu huki akieleza kuwa baada ya hapo watakutana wote kwa pamoja na kisha kupeana majukumu ya kazi ya kila idara lakini moja ya mkakati ni kuhakikisha viongozi wa Ngome hiyo wanahamasiaha wanawake kujiunga na Chama hicho kutokana na kutambua wapiga kura waaminifu nchini kwetu ni wanawake.

"Hatuna shaka hata kidogo Ngome ya Wanawake ya ACT Wazalendo tutahakikisha tunasimama kidete katika kuona Chama chetu kinashika Dola.Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu tunataka kuchukua Dola kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar,"amesisitiza Kimwanga na kuongeza uteuzi wa majina hayo umezingatia vigezo na wateule hao wa kamati mbalimbali watatumikia katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Akitaja  kamati hizo na viongozi wake kuwa ni .(Itikadi , Uenezi na Mawasiliano kwa Umma),  Katibu  ni Raya Ibrahim Khamis na Naibu Katibu ni Ashura Ali.

Wakati Kamati ya Mipango na Uchaguzi Katibu ni Mary Boniphace na Naibu Katibu ni Lutfiya Kassim Juma na Kamati ya Uadilifu katibu wake ni Fuata Mussa Mbaraka na Naibu Katibu ni Rabia Omary Kaliji.

Pia amesema kwa kamati ya Fedha, Miradi na Uchumi, Katibu wake ni Khadija Salum Ali na Naibu Katibu ni Chiku Aflah Abwao na kamati ya Jinsia Wanawake Wenye Mahitaji maalum , Raisa Abdallah Mussa na  Naibu wake ni Bahati Hamad Chirwa.

Wakati huo huo Makamu Mwenyekiti wa Ngome hiyo Elizabeth Mfugale amesema kwamba wana imani kubwa sana na safu hiyo hasa kwa kuzingatia wote ambao wameteuliwa wanazo sifa zinazojitosheleza katika kutekeleza majukumu yao kwa maslahi ya Chama chao na Taifa kwa ujumla.

"Lengo na tegemeo kuu la Ngome hii ni kuhakikisha tunaibuka na ushindi wa kishindo na kuongeza idadi ya wanawake viongozi hapa nchini,"amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...