Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akikabidhi ujumbe maalum wa Rais Dkt John Pombe Magufuli kwenda kwa Rais wa Marekani Doland Trump. Anayeshuhudia ni Balozi wa Tanzania Nchini Marekani Balozi Wilson Masilingi
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Marekani Nchini Tanzania Dkt. Donald Wright (aliyevaa tai nyekundu) Kulia ni Balozi wa Tanzania Nchini Marekani Balozi Wilson Masilingi
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ambaye pia anashughulikia masuala ya Afrika Mhe. Tibor Nagy mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Washington,Marekani

***************************

Washington,Marekani,

Tanzania na Benki ya Dunia zimekubaliana kuendelea kushirikiana katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu,uendelezaji wa miundo mbinu na masuala ya kijamii kupitia mikopo,ruzuku na misaada inayotolewa na benki hiyo ili kuisaidia Tanzania kupiga hatua za kimaendeleo na kutokomeza umasikini miongoni mwa raia wake.

Hayo yamebainika baada ya mazungumzo baina ya Mkurugenzi mtendaji wa benki ya Dunia anayeiwakilisha Marekani Dkt. Jennifer “DJ” Nordquist na Mjumbe maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi mazungumzo yaliyofanyika katika makao makuu ya Benki hiyo Washington Marekani ambapo wamejadili masuala mbalimbali hususani kuhusu masuala ya mahusiano baina ya Benki ya dunia,Marekani na Tanzania.

Pia wamezungumzia masuala mbalimbali ya miradi maendeleo ikiwa pamoja na sekta ya elimu na kujadili maeneo mbalimbali ambayo Benki hiyo imeisaidia Tanzania aidha kwa mikopo ya masharti nafuu au misaada ikiwa ni pamoja na ujenzi na uendelezaji wa shule za msingi na sekondari.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeiwakilisha Marekani Dkt. Jennifer “DJ” Nordquist amesema anafuatilia kwa ukaribu masuala yote yanayoendelea Tanzania na kwamba anavutiwa na mambo ya maendeleo yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli katika utoaji wa elimu bure kwa shule za msingi na sekondari.

Aidha Dkt Jennifer “DJ” Nordquist ameeleza kufurahishwa kwake na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali na kusisitiza kuwa ni vyema elimu inayotolewa isiwe na ubaguzi na kuahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania kuoata fedha ziatakazowezesha kuboresha miundombinu ya elimu nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mabweni katika shule za kata na kutoa mfumo maalum wa utoaji wa elimu kwa wanafunzi wanaokatisha masomo kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na wale wanaopata ujauzito.

Mkurugenzi Mtendaji mbadala wa Kanda Namba 1 ya Afrika kutoka Benki ya Dunia Bw. Taufila Nyamadzabo amesema mazungumzo baina ya Tanzaia na benki ya dunia yamekuwa ni ya manufaa kwa kuwa yameondoa sintofahamu iliyokuwepo kati ya pande hizo mbili na ni matumaini yake mradi huo utapitishwa na bodi ya benki ya dunia hivi karibuni.

Katika tukio jingine Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masharki Prof. Palamagamba John Kabudi amewasilisha ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kweda kwa Rais wa Marekani Mhe. Donald Trump kupitia Wizara ya mambo ya Nje ya Marekani.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ambaye pia anashughulikia masuala ya Afrika Mhe. Tibor Nagy ndiye aliyepokea ujumbe huo na kuahidi kuendeleza mashirikiano mazuri nay a muda mrefu yaliyopo kati ya Tanzania na Marekani. Katika mazungumzo hayo Naibu Waziri huyo ameambatana na Balozi Mteule wa Marekani Nchini Tanzania Dkt. Donald Wright

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kwa hiyo waliopatwa na mimba wakiwa shule watapata nafasi ya kusoma tena? Msrekani ndiyo baba lao kweli,hivi vingine ni vimbuzi jike tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...