Na Said Mwishehe, Michuzi TV

RAHA Liquid Telecom inayojihusisha na utoaji wa huduma ya intanet imesema katika kipindi hiki ambacho Dunia inaendelea kupambana dhidi ya virusi vya Corona, wao wanaongozwa na imani kila mtu kwenye Bara la Afrika ana haki ya kuungwanishwa na huduma ya intanet

Imesema kadri zinapochukuliwa hatua dhidi ya maambukuzi ya COVID-19 (Coronavirus), wanakumbuka mahitaji yanayoongezeka na hivyo mtandao wa uhakika na uwezo wa kufanya kazi majumbani, kujifunza na matumizi ya kijumla.

Taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa Raha Liquid Telecom Hussein Kitamba aliyoitoa leo Machi 31 mwaka 2020 kwa vyombo vya habari amesema wanafurahi kuwapatia wateja wao wa thamani kupata suluhisho pamoja na familia zao kwa kuhakikisha wanatoa huduma bora ya intanet kwa ajili ya kuwezesha shughuli za kiuchumi na mawasiliano mbalimbali kuendelea kufanyika.

"Kama mteja wetu wa thamani,Raha Liquid Telecom iko hapa kukusaidia na changamoto hii. Intaneti yetu isiyokuwa na kikomo itakuwezesha kuendelea na kazi, kujifunza na kupitia vipindi vya familia. Ofa hii itakuepo kwa mwezi mmoja tu, hata hivyo, tutaendelea kufuatilia hali hii tukiwa pamoja na kukushauri ipasavyo. Tunatambua kwamba wakati huu ina changamoto, na tunataka mtambue kwamba Raha Liquid Telecom ipo kwa ajili yenu,"amesema Kitambi.

Ameongeza kuwa " Utaunganishwa na intanet ya mbs 5 kwa Sh.100,000 bila gharama za ufundi kwa saa 48 na hii ni kuhakikisha namba kubwa ya watanzania wanaungwanishwa na huduma iliyo kasi ya intanet, kwa wafanyakazi wenzao na wanafamilia".

Amefafanua kuwa suluhisho makazini kwa biashara jaribio la bure la miezi sita kupitia Microsoft Office 365 na Teams Microsoft ambazo zinalenga kuleta mabadiliko jinsi mashirika yanavyofanya kazi, kuungana na kupata manufaa wakati ukiwa nje ya ofisi na kwa wanaotaka kuelewa zaidi wanaweza kutembelea tovuti ya www.liquid.fyi.virtual.

Kitamba amesema suluhisho katika elimu ni kufunga intanet katika taasisi za elimu bila gharama zozote na kwamba wanatarajia kuwa na Microsoft Office 365 Elimu, Microsoft Teams, kuleta mabadiliko katika elimu jinsi madarasa yanavyofanya kazi pale wanapokua nje ya madarasa.

"Nieleze tu hatutawaacha nyuma wateja wetu wa HAI kwa sasa kwani tunaendelea kuwapatia suluhisho la hali ya juu na ofa za juu zaidi. Kuanzia Machi 23 2020, tulieboresha usajili wa Hai Home internet na uwezo wake umekua mara mbili zaidi kwa mfano usajili wa 5mbps moja kwa moja unajiboresha kuwa 10mbps,"amesema.

Ameongeza kuwa Promosheni hiyo ilitakiwa kumalizika Machi 30 lakini imepelekwa mbele zaidi na sasa wateja wote wanaweza kufurahai mara mbili zaidi ya uwezo wa intaneti na mwezi wa ziada wa usajili na kwamba wanaendelea kutoa huduma zenye ubora na za kisasa na suluhisho wakati tukiendelea kuwa karibu na wateja wetu kuwa na biashara na elimu endelevu kwakati huu.

"Wote tuwe macho hata tunapokuwa katika maisha yetu ya kila siku kwa usalama na tujisikie huru kuwafikia Raha Liquid Telecom kwa msaada wowote na mwongozo,"amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...