Wafanyabiashara wawili raia wa India waliohukumiwa leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wamehukumiwa  kutumikia kifungo cha nje kwa mwaka mmoja na kulipa faini ya sh. Milioni 230 baada ya kukiri shtaka moja lililokuwa linawakabili la kukutwa na mazao ya misitu (magogo) yenye thamani ya sh. Milioni 505.1 bila ya  kuwa na kibali cha wakala wa Misitu, (TFS).
Baadhi ya Magogo yaliyo kwenye makontena ambayo walikutwa nayo wafanyabiashara wa nchini India.

Na Karama Kenyunko globu ya jamii. 
MAHAKAMA ya Hakimu Kisutu imewahukumu wafanyabiashara wawili raia wa India kutumikia kifungo cha nje kwa mwaka mmoja na kulipa faini ya sh. Milioni 230 baada ya kukiri shtaka moja lililokuwa linawakabili la kukutwa na mazao ya misitu (magogo)  yenye thamani ya sh. Milioni 505.1 bila ya  kuwa na kibali cha wakala wa Misitu, (TFS)

Aidha mahakama imeamuru kutaifishwa kwa magogo hayo yaliyohifadhiwa kwenye makontena 18 katika Bandari kavu Ubungo kuwa mali ya serikali.

Wafanyabiashara waliohukumiwa ni Manish Khattar na Rajesh Velram wameamriwa kulipa fidia hiyo baada ya kufika makubaliano na mwendesha mashtaka wa serikali DPP kufuatia makubaliano na kukiri makosa yanayowakabili.

Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega baada ya kujiridhisha na vielelezo vilivyo wasilishwa na upande wa mashtaka uliokuwa ukiongozwa na wakili wa serikali mwandamizi Renatus Mkude baada ya mahakama kuhamia eneo la Ubungo vilipohifadhiwa vielelezo hivyo.

Akisoma hukumu hiyo leo Machi 26, 2020  katika eneo la bandari kavu jijini Dar es Salaam, Hakimu Mkazi Mkuu Janeth Mtega amesema washitakiwa wametiwa hatiani kwa kosa la kupatikana na mazao ya misitu aina ya magogo isivyo halali.

Alisema kufuatia kosa hilo anawahukumu kila mmoja kulipa faini ya Sh. Milioni 115 na kutumikia  kifungo cha nje cha miezi 12 huku wakitakiwa kutokufanya kosa lolote la jinai katika kipindi hicho.

Katika kesi hiyo washitakiwa wanadaiwa kati ya Januari 15, 2015 na Oktoba 31 mwaka huu, katika eneo la NASACO lililopo Ilala jijini Dar es Salaam kwa pamoja walikutwa na magogo yenye thamani ya Sh. Milioni 505.1 bila kuwa na kibali kutoka Wakala wa Misitu.

Hata hivyo washitakiwa hao wamelipa faini hiyo na kuachiwa huru.

Washitakiwa hao baada ya kufanya mazungumzo na DPP walifutiwa mashitaka sita yakiwemo ya kuongoza genge la uhalifu, kughushi, kutakatisha fedha na kukwepa kodi na kisha kubakishwa na shitaka moja la kupatikana na mazao ya misitu aina ya magogo isivyo halali.

Awali kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Mawakili wa Utetezi wakiongozwa na Shabani Mlembe, Lightness Minja na Alfredy Affa waliiomba mahakama kuwapatia wateja wao adhabu nafuu kwa kuwa bado wanategemewa na wafamilia zao, ni kosa lao la kwanza lakini pia awajaisumbua mahakama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...