Bi Ellen Johnson Sirleaf Rais wa zamani wa Liberia Jumapili ijayo ataanzisha mpango wa kuwasaidia wanawake wa Kiafrika kufikia nyadhifa za juu katika bara hilo linalodhibiwa na marais wanaume.
Bi Sirleaf ambaye ni mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2006 alikuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa rais wa nchi barani Afrika mwaka 2006. Aliondoka madarakani mwaka 2018 katika nchi ya Liberia iliyowahi kuathiriwa na vita kupitia mchakato wa kwanza wa amani wa kukabidhi madaraka nchini humo katika kipindi cha miongo saba.
Amesema kuwa wameamua kuanzisha wimbi hilo la wanawake ambao wapo tayari kushika nyadhifa za ngazi za juu katika jamii na kwamba wanawake hao pia watashika nyadhifa hizo katika ngazi ya kimataifa bila ya haya wala bughudha.
"Baaada ya miaka mingi ya kujaribu kupata uongozi wa ngazi za juu nimepata tajiriba na uzoefu mkubwa wa namna jambo hilo huwawia gumu wanawake", amesema Bi Ellen Johnson Sirleaf ambaye alikuwa mtu wa tano kushinda Tuzo ya Uongozi Bora ya Mo Ibrahim barani Afrika mwaka 2017.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...