NA TIGANYA VINCENT
MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ameuagiza uongozi wa Halmashauri
ya Manispaa ya Tabora kuhakikisha wanafunga Mfumo wa ukusanyaji wa
mapato kwa katika maeneo yote yanayosuka na utoaji wa huduma za afya
ili kuongeza kiwango cha ukusanyaji mapato.
Ukusanyaji wa mapato kwa njia za stakabadhi zilizo katika vitabu
zimesababisha baadhi ya mapato kupotea na mengine kuishia mifukoni mwa
watumishi wasio waaminifu.
Mwanri ametoa kauli hiyo jan20a wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa
shughuli za Malipo kwa Ufanisi (RBF) kwenye Vituo na Zahanati mbali
katika Manispaa hiyo.
Alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Tabora kuhakikisha Vituo
vyote na Zahanati zote zinafungwa mfumo wa Serikali wa ukusanyaji wa
mapato katika Hospitali mapema iwezekavyo.
Naye Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu alisema kitendo cha
Vituo na Zahanati kuendelea kukusanya mapato kwa mfumo wa zamani ni
kinyume na agizo la Serikali lililotolewa mwaka 2016.
Alisema tangu mwaka huo hadi 2020 bado kuna Zahanati na Vituo vya Afya
vinaendelea kukusanya fedha kwa kutumia stakabadhi za zamani jambo
ambalo wakati mwingine linasababisha kuzalishwa kwa Hoja za Kiukaguzi.
Makungu alisema sehemu zilizofunga mfumo wa ukusanyaji wa mapato kwa
Mtandao umesaidia kuongeza mapato mara mbili akitoa mfano wa Hospitali
ya Rufaa ya Kitete ambapo makusanyo yameongezeka kutoka milioni 30 kwa
mwezi hadi kufika 60.
Alisisitiza ni lazima Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali zote
zifunge mfumo wa ukusanyaji wa mapato ili ziwe kupata fedha ambazo
zitawawezesha kujitegemea ifikapo 2025.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akizungumza jana na wagonjwa
katika Zahanati ya Ng’ambo wilayani Tabora wakati wa ziara ya ukaguzi
wa utekelezaji wa shughuli za Malipo kwa Ufanisi (RBF) kwenye Vituo na
Zahanati mbali katika Wilayani humo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...