NA TIGANYA VINCENT,TABORA

MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa huo kutoa taarifa za wageni wasiofahamika walikopotoka pindi wanaonekana katika maeneo yao ili kuepuka kuambukizwa homa kali ya mapafu inayoenezwa na kirusi kipya aina ya Corona.

Alisema Mkoa huo ni mkubwa na unapatakana na mikoa inayopakana na Nchi za jirani na upo uwezekano wa wageni kuingia kwa kutumia njia za panya na hivyo kuhatarisha afya za wakazi wa Tabora.

Mwanri alitoa kauli hiyo leo wakati alipokuwa akifungua mkutano wa timu ya Mkoa wa Tabora ya kudhibiti janga la Corona lisiingie mkoani humo.

Aliwahimiza wananchi kuendelea kuchuka taadhari dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayoenezwa na kirusi kipya aina ya Korona kwa kunawa mikono mara kwa mara.

Aidha Mwanri aliwataka wananchi kususia maduka yote ambayo wamiliki wake watakutwa hawaweka vitakasa mikono ama ndoo kwa ajili ya wateja kunawa kabla ya kununua bidhaa.

Mwanri alisema wamiliki wa aina hiyo wana nia mbaya na Watanzania na wanapingana na maagizo ya viongozi wa Kitaifa na wataalamu ya kuwataka wananchi kuna mikono kama kinga ya janga la Corona.

Amevitaka vyombo vya habari na Redio zilizomo mkoani humo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya kujikinga na janga la corona ili Mkoa huo uendelee kuwa salama.
 Mkuu wa Tabora Aggrey Mwanri akifungua leo mkutano wa Timu ya Mkoa huo ya kudhibiti ugonjwa wa Corona.

 Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akitoa maelezo juu ya majukumu ya timu ya Mkoa wa kudhibiti ugonjwa ya corona.Picha na Tiganya Vincent
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...