Kulia ni Muwakishi wa rais Redcross Taifa Ndg Japhet Shirima akikabidhi msaada kwa mzee Asanterabi Shoo ambae ni miongoni mwa waathirika wa mafuriko eneo la mto wa mbu wilayani Monduli kufuatia Mvua zinazo endelea kunyesha katika baadhi ya maeneo nchini.
Timu ya chama cha msalaba mwekundu wakiwa katika Kata ya Mto wa Mbu mkoani Arusha.
Dora Mushi-Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba mwekundu mkoani Arusha akizungumza na baadhi ya wananchi wa Mto wa mbu waliopatwa na madhila ya mafuriko.
Na,Vero Ignatus -Arusha
Familia zaidi ya 150 zilizoathiriwa na mafuriko ya mvua katika eneo la mto wa mbu wameiomba Serikali kuwatafutia mahali pa kuishi ili kuweza kujinusuru na adha ya hiyo kufuatia mvua zinazo endelea
Wakizungumza baadhi ya wazee na walemavu ambao kwasasa hawana mahala pa kuishi kufuatia adha hiyo huku wakaiomba serikali kupata eneo salama la kuishi kama wanavyo eleza mzee Asanterabi shoo na bi Mariam Mboya kwamba wao wapo tayari kuhama kama serikali itawapa eneo la kujenga kwasababu viwanja kwa sasa ni walipo sasa ni bondeni
Akizungumza kwa niaba ya Rais wa Chama cha msalaba mwekundu taifa baada ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali ikiwemo magodoro na huduma muhimu kwa wakina mama vyenye thamani ya shilingi milioni 25,Japhet Shirima anaeleza kuwa wameamua kuwafariji watu waliopatwa na mafuriko mto wa mbu kama dhima ya chama chao inasema ni kufanya kazi kwa nguvu ya binadamu
''Chama cha Msalaba mwekundu kimeamua kuwafariji watanzania wenzetu ili kuwapunguzia machungu yaliyowapata kutokana na mafuriko na tumewalete vitu vichache vya nyumbani kama vile magodoro,ndoo,sufuria ,mablanketi kwaajili ya matumizi ya nyumbani"Alisema
Amewataka wananchi kuchukua tahadhari na kuepuka kukaa maeneo hatarishi na wakae maeneo yaliyo salama zaidi ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza,ili kujikinga na majanga hayo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha msalaba mwekundu mkoani Arusha Dora Mushi amewasihi wananchi kujiunga na chama hucho kwani ni kitengo kisaidizi cha serikali
kinachohamasisha ili kuwafikia watu kwa karibu pale yamapotokea majanga
Amesema wananchi wanapojiunga katika Chama cha msalaba mwekundu zaidi wanawashauri namna ya kuishi,kujikinga na majanga kwani ndiyo wanaotoa huduma ya kwanza kabla pale tatizo linapotokea katika jamii
"Hivyo katika Kata hii ya na Mto wa Mbu tumewaweza kuhamasisha wameweza kujiunga wanachama 60 na tumetenga siku maalumu kwaajili ya kuja kuwapatia elimu namna ya kutoa huduma ya kwanza linapotokea tatizo katika jamii"
Kufuatia mvua zinazo endelea kunyesha wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari za makusudi ikiwa ni pamoja na kuhama katika maeneo hatarishi ili kujiepusha na maafa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...