WAMJW – Dar es Salaam
Serikali imepokea msaada wa vifaa kinga kutoka China kwa ajili ya kusaidia kukabiliana na mlipuko wa maambukizi ya homa kali ya mapafu inayoambukizwa na virusi vya Corona (COVID-19) kutoka taasisi ya Jack Ma na Alibaba.
Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Serikali, Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Muhammed Bakari Kambi amesema msaada huo ambao umetolewa na Taasisi ya Jack Ma na Alibaba ni pamoja na mavazi (PPE) 1,000 ya kujikinga wakati wa kuhudumia watu waliobainika kuwa na ugonjwa huo ni pamoja na vitendanishi (Rapid Tests) 20,000 na Barakoa (Masks) 100,000.
Prof. Muhammed amesema msaada huo utawasaidia wataalamu wa afya nchini wakati wa kuwahudumia waliobainika na watakaobainika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona.
“Tunashukuru kwa msaada huo kama serikali,tumekuja hapa kushuhudia sehemu ya shehena ya tani tatu ya vifaa-tiba vilivyotolewa na Taasisi ya Jack Ma (Alibaba) ambavyo vimewasili usiku wa leo na ndege ya mizigo ya Jamhuri ya Shirikisho la Kidemokrasia Ethiopia,” amesema Prof. Muhammed.
Katika hatua nyingine, Prof. Muhammed amemshukuru Afisa Ubalozi wa Jamhuri ya Shirikisho la Kidemokrasia Ethiopia Ndg. Tewodros Girma ambaye amekabidhi msaada huo kwa niaba ya Balozi wa nchi hiyo, Mhe. Yonas Yosef.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...