Na Amiri kilagalila,Njombe

Mbunge wa viti maalum mkoani Njombe kupitia chama cha mapinduzi Mhe, Neema Mgaya amekabidhi Kompyuta kumi zenye thamani ya milioni 17,370,000/=.kwa baadhi ya shule za sekondari mkoani Njombe ili kuboresha na kuinua taaluma katika mkoa huo.

Aidha mbunge huyo ametoa Printer mbili zenye thamani ya Tsh milioni 1,905,062, kebo nane kwaajili ya Umeme zilizogharimu kiasi cha Tsh, lakimbili na kufanya jumla ya vifaa vyote alivyovitoa katika ziara hiyo kufikia kiasi cha Tsh Milioni 19,475,062.

Kompyuta hizo na Printa amekabidhi kwa Shule ya Sekondari Ludewa Wilayani Ludewa na shule ya Sekondari Wanging'ombe Wilaya ya Wanging’ombe, huku akisema lengo ni kuwawesha Walimu kufundisha na Wanafunzi kujisomea kwa njia ya Mtandao na kuahidi kufunga Mtandao wa Intaneti katika Shule hizo kwa gharama zake.

Ili kuwatambua Watoto wenye mahitaji Maalumu wanaosoma katika Shule maalumu Mundindi Wilayani Ludewa Neema Mgaya amemkabidhi Afisa Elimu Sekondari Wilayani humo Fedha kiasi cha Tsh 70,000/= kwaajili ya kununua Mahindi ili yatumike kwa chakula cha Wanafunzi wa Shule hiyo.

Matenus Ndumbaro Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Ludewa licha ya kumshukuru Mhe, Neema Mgaya amesema Vifaa hivyo vitaongeza mbinu za ufundishaji na kukuza kiwango cha ufaulu wa Wanafunzi Wilayani humo kwakuwa watapata mbinu mpya kupitia Mtandao wa Intaneti.

Bi, Monica Mchilo Diwani wa Kata ya Ludewa pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Ludewa pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bw, Paul Matunduru wameahidi kuvitumia vyema vifaa hivyo na kuvitunza ili viweze kutumika kwa muda mrefu zaidi.

“Tunamshukuru Mhe, Neema Mgaya kwa Vifaa hivi tunaahidi kuvitunza ili vidumu katika Shule yetu kwa faida ya Wanafunzi na Walimu ambao watasoma na kufundisha kwa njia ya Mtandao wa Intaneti pia itasaidi kukuza kiwango cha Ufaulu kwenye shule yetu” Mwalimu Matunduru.

Kwa Upande wake afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Wanging'ombe Bi, Loyce Mgonjwa na Diwani wa Kata ya Wanging'ombe Wilayani humo Mhe, Geofrey Nyagawa wamekiri kupokea Kompyuta hizo na Printa huku wakimshukuru Mhe, Neema Mgaya kwa kuunga mkono Juhudi za Serikali katika kuboresha Miundombinu ya Elimu. "Hii ni hatua kubwa ya kuboresha sekta ya Elimu katika Wilaya yetu na Mkoa wa Njombe kwa ujumla, tunampongeza sana Mhe, Neema Mgaya kwa kutoa Vifaa hivi ili kuboresha Sekta hii muhimu ya Elimu"Bi, Mgonjwa Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Wanging'ombe.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...