Na Pamela Mollel, Arusha

Taasisi na makampuni binafsi wameaombwa kuchangia vifaa mbalimbali kwaajili ya kusaidia kupambana na ugonjwa wa Virusi vya Corona (Covid - 19)ambao hivi sasa unaleta mtikisiko wa kiuchumi

Aidha wataalam na makada wa afya zaidi ya 525 wamepewa mafunzo elekezi juu ya kukabiliana na ugonjwa wa Corona

Rai hiyo imetolewa jana Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Hargeney Chitukuro wakati alipokuwa akifungua kikao kazi cha wataalam wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii katika kutekeleza mkakati wa kuelemisha jamii kuhusu ugonjwa wa Korona yaliyofanyika Mkoani Arusha

Chitukuro alisema endapo Taasisi na makampuni binafsi yakijitokeza kuchangia vifaa mbalimbali kwaajili ya kupambana na ugonjwa huo kutasaidia kuwapa ahueni wagonjwa watakaobainika kuwa na ugonjwa huo na kuwekwa karantini

Alisema hospitali ya Mount Meru kunaeneo maalum limetengwa huku serikali ya Mkoa wa Arusha ikiwa imepata eneo kwaajili ya kujenga hospitali itakayokuwa inatibu ugonjwa huo

"Tunaomba Taasisi na kampuni mbalimbali wajitokeze kuchangia vifaa kwaajili ya kudhibiti ugonjwa huu ambao kwa sasa umekua tishio Duniani na kuepelekea sgughuli baadhi kusitishwa kwa muda "

Aliongeza kuwa wanahitaji vifaa mbalimbali zikiwemo oxgen na vingine kwaajili ya kusaidia wagonjwa watakaoumwa ugonjwa huo nchini

Awali Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii, Wizara ya Afya, Patrick Golwike alisema mafunzo hayo ni endelevu na kwakuanzia wametoa elimu hii Mkoani Arusha na Dar es Salam yenye lengo la kuhakikisha jamii inachukua hatadhari dhidi ya ugonjwa huo.

Alisema mafunzo hayo yameshirikisha maafisa hao kutoka halmashauri za Wilaya za Ngongoro, Karatu, Longido na Monduli.


Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Bw. Hargeney Chituturo akizungumza wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuelimisha jamii kuhusu ugonjwa wa Corona Maafisa Ustawi na Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Arusha, katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha jana tarehe 28/03/2020.
Maafisa Ustawi na Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Arusha wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuelimisha jamii kuhusu ugonjwa wa Corona katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha jana tarehe 28/03/2020.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya jamii Wizara ya Afya Bw. Patrick Golwike akitoa mada ya namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kwa Maafisa Ustawi na Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Arusha, katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha jana tarehe 28/03/2020.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...