
Tasnia ya urembo na vipodozi nchini imepigwa sana na tishio la Corona nchini. Ingawa serikali imetangaza kufungwa kwa vyuo vikuu na mashule, maafisa wa afya bado hawajatoa miongozo au kuamuru vizuizi vyovyote kuhusu saluni za nywele, wakiwemo vinyozi, watengenezaji kucha, makeup artists nakadhalika. Chama cha Urembo na Vipodozi Tanzania (TCA) inajitahidi kutoa elimu ya kujilinda kwa virusi vya Corona kwa wanachama wake lakini inaona gap kubwa iliyopo ambapo elimu hii yapaswa kuwafikia wenye masaluni nchi nzima ili wafanyakazi wa masaluni na wateja wao wajue namna ya kujilinda na virusi vya Corona - na kusaidia kuzuia kuenea kwa virusi hivi hatari.

Mwenyekiti wa TCA, Shekha Nasser amekuwa akiongea kuhusu wasiwasi wake juu ya wenye masaluni kuweza kujisaidia kifedha na familia zao ikiwa amri ya kufunga masaluni yote nchini itatoka. "Hatuwezi kumhudumia mteja kwenye masaluni kwa umbali wa mita moja wakati wa kumtengeneza kucha au nywele, ni kitu ambacho hakiwezekani kabisa," alisema Shekha.TCA imewaasa wanachama wake na wenye masaluni kote nchini kuchukua tahadhari na kuiomba serikali kuangalia itaweza kusaidia wamiliki wa masaluni, makampuni na wafanyikazi wanaoshughulikia janga la corona virus. Tasnia ya Urembo na Vipodozi ni moja ya sekta kubwa nchini iliyoajiri vijana wengi wa kike na wa kiume ambao vipato vyao vinategemewa katika kuhudumia familia zao kila siku.

Corona virus inaumiza huduma, muda na fedha za wafanyakazi walio amua kujitenga “Social distancing” kwani njia kubwa ya kujikinga ni kulazimika kukaa nyumbani na kujitenga. TCA inawaomba wenye masaluni kote nchini kuvumilia, kuwa watulivu na kumuomba Mwenyezi Mungu kwani hali hii ni hatari sana na ni janga la dunia.
Kama tulivyosikia maafisa wa serikali wametoa kote amri ya kuzuia msongamano wa watu kwenye mabaa, mikahawa, mazoezi, na biashara zingine kuzuia kuenea kwa COVID-19, ugonjwa unaosababishwa na virusi vya maji maji. Hata hivyo watengenezaji wa nywele, kucha na wamiliki wa saluni bado hawajapigwa marufuku katika kazi zao hivyo wanalazimika kuamua wenyewe kuendelea kufanya kazi katika biashara zao huku wakichukua tahadhari na kufuata maelekezo ya wizara ya afya.
Kwa wale wenye masaluni walio amua kufunga, ni uamuzi ambao utakata chanzo chao cha mapato pekee kwa kile kinachoweza kuwa wiki au hata miezi ijayo. "Sekta yetu kwa jumla imeachwa nyuma kidogo katika kuwapa elimu kwa wajasiriamali wadogo wenye masaluni kwa sababu hatujapewa dhamana kutoka kwa serikali au maafisa wa serikali kuwa tunapaswa kufunga," alisema Shekha Nasser, Mwenyekiti wa TCA.
Hatujapewa maagizo maalum ya kufunga, lakini, namaanisha, kutokana na uelewa wa kila mtu, mahali pa kazi na mazingira yetu, ni, kama maeneo ya kuenea huu ugonjwa, alisema Sada Abdallah, mmilikiw wa salon Mikocheni, Dar es Salaam. Wengine wanaamua kuendelea kufanya kazi hadi serikali au wizara ya afya itakapowalazimisha kufunga - na wanaendelea kufanya kile wanachoweza ili kudumisha usafi maha
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...