KAMATI ya Amani mkoa wa Morogoro imesema kuwa elimu ya utumiaji wa huduma za mawasiliano imefika kwa wakati mwafaka kutokana na teknolojia hiyo kukua kila siku.

Wameyasema hayo wakati wa Semina ya Kamati ya Amani ya Mkoa  Morogoro inayotolewa na  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kutoa elimu juu ya utumiaji wa huduma za mawasiliano kwa kujinga na Uhalifu unapotumia huduma hizo.

TCRA ipo katika Kampeni ya SIRUBUNIKI kuwa Mjanja ambayo inakwenda katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani katika kutoa elimu hiyo utumiaji wa huduma za mawasiliano.

Akizungumza katika Semina hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano wa Kamati ya Amani Mkoa wa Morogoro Juma Ng'ondavi amesema kupata Semina ya huduma za mawasiliano kuna umuhimu kutokana na wao wanazunguka jamii yote ya Mkoa huo.

Amesema kuwa Kazi yao ni pamoja kuwa mabalozi kwa viongozi ambao hawajafika kuendelea kutoa elimu katika ibada ili waumini waweze kupokea elimu ya kujikinga na uhalifu wakati unapotumia huduma za mawasiliano.

 Katibu wa Makanisa Mkoa wa Morogoro na Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano Mkoa huo Mchungaji Canon Regnald Mdugi amesema  elimu waliopata TCRA wataipeleka kwa waumini kwa kuhakikisha wanaelewa katika kujikinga na uhalifu wakati kutumia mitandao ya mawasiliano.

Amesema viongozi wa dini kazi yetu ni kuitumia elimu hii na  kuipeleka  kwa waumini  kwa ustawi  wa nchi yetu

Kampeni ya  kuelimisha jinsi ya kujikinga na uhalifu wakati wa kutumia huduma za mawasiliano  ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Sirubiniki Mjanja  haingizwi  chaka  inayolenga  katika kuelimisha umma ya kujikinga.


 Wakichangia  katika semina hiyo viongozi hao wamepongeza juhudi  za Mamlaka ya Mawasiliano za kuwalinda  wateja na kuahidi  kushiriki katika  kampeni  hiyo.

Kamati hiyo imetoa wito  kwa taasisi kuiga mfano  wa TCRA katika  kuelimisha viongozi wa dini wanawafuasi wengi  na ushawishi  mkubwa  katika   jamii.

Kampeni  ya Sirububiki  Mjanja haingizwi  chaka  imeandaliwa  na Mamlaka ya Mawasiliano  kushirikiana na Jeshi  la polisi  kitengo cha uhalifu  mitandaoni  yenye lengo la kuelimisha  jamii jinsi ya kujikinga  ili wasirubuniwe wanapotumia  huduma za mawasiliano.

 Kampeni  ya Sirububiki Mjanja haingizwi chaka  inalenga kuzifikia kamati za Amani za mikoa yote ya Tanzania
 Kamati za Amani za mikoa ni kamati za viongozi wa dini na madhehebu  mbalimbali ambazo zimeundwa kwa lengo  la kujenga  maridhiano kwa watu wa dini mbalimbali

Nae Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Christopher John amesema kuwa viongozi wa dini ni watu mhimu sana katika kutoa elimu kwa waumini.

Amesema kuwa huduma za mawasiliano ni pana na teknolojia yake inabadilika kila siku 

John amesema TCRA itaendelea kutoa elimu kuhusiana na matumizi ya Mawasiliano kuhakikisha yanakuwa salama  kwa ustawi wa nchi.

Nae Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi amesema kuwa wanafikia makundi yote katika Kampeni ya Sirubuniki kuwa Mjanja.
Amesema wakati amefikia wa kutumia mawasiliano kwa kulinda usalama wa nchi  pamoja na wanaotumia mawasiliano bila kufuata sheria na taratibu mkono wa sheria utawakuta.
 Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) akizungumza wakati wa Semina ya Kamati ya Amani ya Mkoa Morogoro kuhusiana utumiaji wa huduma za Mawasiliano ikiwa ni Kampeni ya Sirubuniki kuwa Mjanja.
 Katibu wa Umoja  Makanisa Mkoa wa Morogoro,Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano Mkoa huo  Mchungaji Canon Regnard Mdugi  akichangia mada katika Semina ya Kamati ya Amani Mkoa wa Morogoro.
 Juma Yahaya Ng’ondavi - Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano Mkoa Morogoro akichangia Semina ya Kamati Amani Mkoa wa Morogoro iliyotolewa na TCRA.

 Kaimu Katibu wa Mkoa wa  Baraza la Miskiti Tanzania  (Bamita) Abdul Koba akizngumza katika Semina ya Amani Mkoa wa Morogoro iliyotolewa na TCRA kuhusiana na utumiaji wa huduma za mawasiliano.




Viongozi wa Kamati ya Amani Mkoa wa Morogoro wakiwa katika Semina ya TCRA kuhusiana na utumiaji wa huduma za Mawasiliano ikiwa ni Kampeni Sirubuniki kuwa Mjanja.
Next
RAIA WA CAMEROON AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA SH. MILIONI 100 AMA KWENDA JELA MIAKA MITATU
Previous
RC MAKONDA ATANGAZA DAWA KWA WAKANDARASI WANAOKIUKA TARATIBU ZA MIKATABA * RC Makonda asema hakuna mgonjwa wa Covid 19, awataka wananchi kufuata maelekezo Na Leandra Gabriel, Michuzi TV MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametangaza kamati ya watu kumi na watatu kutoka Serikali na sekta binafsi ambao watapitia mikataba yote iliyosainiwa jijini humo na kushauri nini kifanyike na hiyo ni pamoja na kuweka wazi mikataba yote ya utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo iliyosainiwa ili wananchi waweze kutambua ni nani anakwamisha utekelezaji wa miradi hiyo ambayo ni muhimu kwa kwao lakini utekelezaji wake umekuwa wa kusuasusa kwa kiwango kikubwa. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuwa kumekuwa na changamoto kubwa ya katika Mkoa hasa kwa wakandarasi wanaoshinda tenda za utekelezaji wa miradi mbalimbali lakini utekelezaji wake umekuwa wa kusuasusa na kuchelewa. "Licha ya kuwakamata na kuwaweka ndani bado kuna mikataba iliyosainiwa na pesa zimetolewa ila miradi haiendi, kwa mfano mto Ng'ombe mkandarasi amepewa zaidi ya bilioni nne lakini hadi sasa mradi umefika asilimia 6 tuu huku akitumia asilimia 60 ya muda wake" Ameeleza Makonda. Amesema kuwa timu hiyo ya watu 13 kutoka serikalini na sekta binafsi watashauri nini kifanyike ikiwemo kuhakikisha mikataba inawekwa wazi, ili kila mwananchi ajue mkataba umesainiwa na nani, anayesimamia ni nani pamoja na muda wa utekelezaji hali itakayowasaidia wananchi kufahamu nani anakwamisha utekelezaji wa mikataba hiyo. Amesema hadi sasa mikataba yote imekusanywa na baada ya kamati hiyo kukaa na kujadili mikataba isiyo na tija na baaifu itavunjwa kisheria. Kuhusiana na mlipuko wa virusi vya Corona (Covid 19) Makonda amesema wananchi wafuate mwongozo uliotolewa na Waziri wa afya Ummy Mwalimu na amewataka wananchi wa Mkoa huo kutokuwa wabishi pindi wanapopewa maelekezo ya namna ya kujikinga na virusi hivyo. " Tuzingatie usafi na namna ya kusalimiana, nashauri tutumie teknolojia ya mitandao ya kijamii kwa umakini hasa kwa kutosambaza taarifa zenye kuleta hofu ya ugonjwa wa Corona, ukiona hali ya dalili toa taarifa na hatua stahiki zitachukuliwa" Amesema kuwa Serikali ipo makini na hadi sasa hakuna aliyegundulika kuwa na virusi hivyo na amewaomba viongozi wa dini kuendelea kukuweka taifa kwenye maombi ili tuweze kulivuka janga hilo lililoikumba dunia. Katika hatua nyingine RC Makonda amezitaka wakala za barabara za TANROAD na TARURA kurejesha miundombinu yote kwa kuwa kuwa fedha za marekebisho takribani shilingi bilioni 165 zimekwishatolewa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...