Wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa Klabu ya Yanga Shija Richard, Salum Rupia na Rogers Gumbo wamejiuzulu nafasi zao leo   ndani ya klabu hiyo.

Hatua hiyo imekuja siku kadhaa baada ya Moja ya wadhamini wa Klabu hiyo kujiondoa kwa madai ya kupangiwa baadhi ya vitu na wajumbe wanne wa kamati ya utendaji.

Sakata hilo liliwafanya wanachama na viongozi wa matawi kumtaka Mwenyekiti wa Klabu hiyo Dkt Mshindo Msolla kuwachukulia hatua kali wajumbe hao.

Katika taarifa wamesema, "Nimeamua kwa hiari yangu kujiuzulu nafasi zote za uongozi katika klabu yangu ya Yanga. Yanga ni kubwa kuliko mimi na kuliko mtu yeyote. Yamezungumzwa mengi lakini mimi sitazungumza chochote. Wakati utaongea,"

Ameeleza zaidi kuwa Ukweli hata usipousema, huwa una tabia ya  kujitokeza wenyewe japo taratibu lakini huwa unadumu milele.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...