Iran imetangaza kuwa hadi sasa watu 552 waliombukizwa ugonjwa wa COVID-19 maarufu kama Corona wamepona na wamepewa ruhusa ya kurudi nyumbani kutoka hospitali.
Akizungumza na waandishi habari Jumatano hii mjini Tehran, Kianoush Jahanpour mkuu wa Idara ya Mahusiano ya Umma katika Wizara ya Afya ya Iran amesema watu hao wote waliopona wako katika hali nzuri hivi sasa.
Ameongeza kuwa, hadi kufikia leo Jumatano adhuhuri kulikuwa na kesi mpya 586 za waliombukizwa kirusi cha Corona kote Iran na hivyo kwa ujumla walioambukizwa ni 2,922. Amesema hadi kufikia Jumatano watu 92 wamepoteza maisha nchini kutokana na kirusi cha Corona. Halikadhalika ametoa wito kwa wananchi wa Iran wasistishe safari zisizo na dharura baina ya miji na pia wajiepusha ni mijumuiko ili kuepusha kuenea ugonjwa huo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...