Benki ya Stanbic Tanzania imemteua Kevin Wingfield kuwa Mkurugenzi Mkuu kuanzia tarehe 01 Aprili 2020.

Wingfield anachukua nafasi ya Ken Cockerill ambae ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Standard Bank nchini Lesotho.

Safari ya Wingfield ilianza mwaka 1998, katika taasisi ya Standard Bank Group, mpaka sasa ana uzoefu wa zaidi miaka ishirini. Wingfield ameshika nyadhifa mbalimbali ndani ya taasisi hiyo ikiwemo; Mkurugenzi wa maendeleo ya kimkakati kwa wateja, huduma za kibenki za watu binafsi na biashara - Standard Bank Africa; Mkurugenzi wa huduma za kibenki za watu binafsi na biashara - Standard Bank Ghana; na Mkurugenzi wa huduma za kibenki za watu binafsi na biashara - Stanbic Bank Uganda.

Katika wadhifa wake huu mpya, Wingfield anategemewa kuongoza ukuaji wa benki, na kuendeleza ubunifu na uvumbuzi ambao utawezesha mafanikio ya kifedha ya watu na biashara nchini Tanzania. Pia kuunga mkono mpango wa kukuza uchumi kupitia uwekezaji katika viwanda na uboreshaji wa miundombinu.

Akizungumza juu ya uteuzi huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Stanbic Tanzania, Mark Mwandosya alisema, “Wingfield anawito wa uongozi, taaluma na uzoefu ambao ameupata kwa kufanya kazi katika masoko mbalimbali barani Afrika. Tunaimani kwamba chini ya uongozi wake, benki hii itaendelea kukua na kuchangia maendeleo ya nchi yetu.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...