Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani  DAWASA wamechukua tahadhari kwa wafanyakazi dhidi ya Maambukizi ya homa ya Mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona.

Dawasa wamechukua tahadhari hiyo kwa kuwapatia wafanyakazi wake wakiwemo mafundi wa maeneo mbalimbali vifaa vya kuwakinga ikiwemo Barakoa ili wavae muda wote wakiwa katika majukumu yao.

Hatua hiyo ni muhimu katika kutii agizo la serikali kwa kuvaa barakoa  ili kuweza kujikinga, kupunguza maambukizi pamoja na kuwalinda wengine pindi wanapotoa huduma kwa jamii.
 Afisa biashara msaidizi  DAWASA  Noel Kipera akisoma mita ya mteja katika eneo la Kimara stop over huku akiwa amevaa (barakoa), kifaa cha kujikinga na maambukizi ya  virusi vya Corona. Dawasa inahakikisha usalama wa watumishi wake dhidi ya maambukizi ya Corona.
 
 ‪Mafundi wa DAWASA Mkoa wa Ubungo wakizibiti uvujaji katika eneo la Mbuzi 40 Kimara kwa kubadilisha mabomba ya nusu inchi. Mafundi hao wametii agizo la serikali kwa kuvaa barakoa kujikinga na  maambukizi dhidi ya virusi vya Corona.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...