NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA

MKUU wa wilaya ya Kibaha,mkoani Pwani Assumpter Mshama ,amewaasa wazazi na walezi kuwakalantin watoto wao kwa kuwasimamia wabaki majumbani,pamoja na kujiendeleza kujisomea pasipo kudhurura magulioni wala mitaani .

Amesema serikali imeshachukua hatua ili kujilinda na corona ,hivyo kuwaacha watoto hao wadhurure badala ya kutulia kujilinda nyumbani itakuwa ni hatari kwa afya zao.

Akiendelea kukumbushia umuhimu wa kijilinda dhidi ya ugonjwa wa corona kwa jamii,Assumpter alisema, pia ngoma na midundiko haina nafasi kwa sasa kujiepusha na mikusanyiko.

Pamoja na hilo,kamati ya maendeleo ya Kata ya Visiga wilayani Kibaha, nayo imetoa elimu ya kujikinga na ugonjwa huo kwa wafanyakazi kwenye viwanda. 

Mtendaji wa kata hiyo ,Aloisia Nyelo alisema kuwa  wamefikia hatua hiyo baada ya kuona kuwa baadhi ya wafanyakazi wa viwandani hawana elimu ya kutosha juu ya maambukizi ya ugonjwa huo.

Alisema kuwa ,pia wametembelea mitaa yote iliyopo kwenye kata hiyo kwa kupitia nyumba kwa nyumba na mkutano na hadi sasa wameshatoa elimu kwa wananchi zaidi ya 15,000 .

Nae Mwenyekiti wa mtaa wa Zegereni Rashid Likunja alisema , janga hilo la Corona ni kama vita hivyo lazima wananchi wote wapate taarifa ndiyo maana wameamua kupita maeneo mablimbali ikiwemo viwandani.

Awali Diwani wa kata Kambi  Legeza alisema kuwa mbali ya kutoa elimu hiyo pia walikagua changamoto ya ubovu wa barabara ya kwenda viwandani kwani ni kero kubwa .

Kamati hiyo ilitembelea viwanda kikiwemo cha cha Gypsum cha BNBM, Hong You Steel Co Ltd na maeneo mbalimbali ya mtaa wa Zegereni.
 MKUU wa wilaya ya Kibaha,mkoani Pwani Assumpter Mshama

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...