Eti Infinix S5pro kuja na sifa tofauti? Kuna madai kwamba Infinix S5pro imechelewa kufika katika soko la Bongo chanzo kikijulikana kama janga la CORONA, na katika kuleta sawa bana ya wateja wa Infinix, Kampuni ya simu ya Infinix imeona si vyema endapo wadau wa Infinix Bongo kupokea Infinix S5pro yenye sifa sawa na zilizopo sokoni kwa sasa nchini India na Pakistani.

Lakini vile vile chanzo chetu kimesema vionjo vilivyofanyiwa kazi kwenye Infinix S5pro vimetokana na comment za wateja kupitia website ya GSMArena kwani kupitia mtandao huo wadau walionekana kuridhishwa na selfie ya simu hiyo yenye megapixel 40 na teknolojia ya kamera kuchomoza ndani ya simu na kukerwa na mfumo wa chaji wakidai ni vyema kwa simu yenye Android V10 (Q) kutumia chaji aina ya TYPE C.

Na kulingana na matakwa ya wateja inasemekana Infinix S5 pro imefanyiwa maboresho mengi kama aina ya chaji na processor pia kuwa yenye speed zaidi ili kuweza kuwafuraisha wachezaji games kupitia simu hiyo lakini pamoja na maboresho yote hayo inasemekana Infinix S5pro itapatikana kwa bei isiyozidi 550,000Tsh ambayo ni sawa na bei ya awali.

Taarifa hizi zinaweza kuwa sahihi au si sahihi ili kuupata ukweli tuwe na subra kwani tarehe 10/4/2020 si mbali. 

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...