Na Said Mwishehe, Michuzi TV

KATIKA kuunga mkono juhudi za Serikali KUHUSU mapambano ya kupunguza kuenea Kwa ugonjwa wa Covid-19,Kampuni ya uuzaji wa vifaa vya ujenzi ya FMJ Hard Ware Lmt iliyopo Buguruni Kisiwani jijini Dar es Salaam imetoa msaada wa vitakasa mikono kwa vyombo vya habari.

Uongozi wa Kampuni hiyo umesema unatambua kazi kubwa inaayofanywa na vyombo vya habari hasa katika utoaji wa elimu na kuhabarisha umma kuhusu Corona, hivyo wameona haja ya kuwawezesha vitakasa mikono hivyo kwa waandishi ili nao wawe salama.

Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wakutoa msaada huo Meneja mauzo wa kampuni hiyo Fredrick Sanga amefafanua wanatambua jitihada za Serikali inazochukuwa kuukabili ugonjwa huo hivyo nao wameona niwakati sahihi kutoa mchango wao japo mdogo kwa vyombo vya habari.

Amesema lengo lao nikuvifikia vyombo vyote vya habari ili kuwapa vitakasa mikono na leo (jana) wameaza kutoa Kwa baadhi ya vyombo vya habari na wengine watafuata.

"Ukweli Kampuni yetu inatambua mchango wa vyombo vya habari katika kuuhabarisha umma wa Watanzania katika masuala mbalimbali yanayotokea nchini.Hata hivyo kwenye hili janga la Corona ambalo limesababisha hofu kubwa kutokana na kusababisha maafa makubwa, tumeona ni jukumu letu kuhakikisha kundi hili la waandishi nalo linakuwa salama kwa kujikinga na maambukizi, "ameeleza Sanga

Pia amesema "Tunaomba kueleza kuwa Kampuni yetu tunaendelea kuungana na Serikali ya awamu ya Tano katika jitihada za kupambana na ugonjwa huo hatari ambao sio tu umesababisha maelfu ya watu duniani kupoteza maisha lakini pia umechangia kukwamisha shughuli za Uchumi.

Sanga ni matumaini yao wadau mbalimbali nchini watajitokeza kwa pamoja kuiunga mkono Serikali kwa kutoa misada ambayo inaweza kusaidia katika kuongeza nguvu kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

" Hivyo Kampuni yetu ya FMJ Ltd, tunawanaomba waandishi kupokea msaaada huo wa vitakasa mikono kwa ajili ya vyombo vya habari na wanaahidi kuendelea kutoa msaada kadri watakavyo jaaliwa na Mungu," amesema. Sanga amesema kuwa wanatoa ushauri kwa kada ya watu wote wanaojishughulisha na uuzaji wa vifaa vya ujenzi pamoja na mafundi ujenzi wote kuendelea kuchukuatahadhari na kufuata maelekezo yanayotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto.

Meneja Mauzo wa Kampuni ya FMJ iliyopo Buguruni Kisiwani jijini Dar es Salaam inayojishughulisha uuzaji wa vifaa vya ujenzi na Fredrick Sanga akizungumza kuhusu uamuzi wa kampuni hiyo kutoa msaada wa vitakasa mikono kwa waandishi wa vyombo vya habari nchini kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na virusi vya Corona.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya FMJ iliyopo Buguruni Kisiwani jijini Dar es Salaam inayojishughulisha uuzaji wa vifaa vya ujenzi na Fredrick Sanga akizungumza kuhusu uamuzi wa kampuni hiyo kutoa msaada wa vitakasa mikono kwa waandishi wa vyombo vya habari nchini kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na virusi vya Corona.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...