Na Amiri kilagalila,Njombe.
Takukuru mkoa wa Njombe imewafikisha mahakamani wilaya ya
Makete maafisa 7 watendaji wa vijiji kwa tuhuma ya wizi wa fedha
Tshs.99,321,466/- za halmashauri ya wilaya ya Makete,ambazo zilikuwa ni
makusanyo ya mapato ya halmashauri kwa kutumia mashine za POS (Point of
Sale electronic Machine)
Mkuu wa Takukuru mkoa wa Njombe Bi.Domina Mukama, amesema kesi zilizofunguliwa mahakamani za maafisa watendaji hao wa
vijiji ni.
1.CC.12/2020 Jamhuri dhidi ya Chrispin Raphael Ngonela
mtendaji wa kijiji cha Matamba wilayani Makete anayeshtakiwa kwa kosa la
wizi wa jumla Tshs. 24,356,656/=
2.CC.13/2020 Jamhuri dhidi ya Exavery Pius Mwabena mtendaji
wa kijiji cha Ikungula wilayani Makete anayeshtakiwa kwa kosa la wizi
wa jumla ya Tshs 3,038,022/=
3.CC.14/2020 jamhuri dhidi ya Elia Mose Nguvila mtendaji wa
kijiji cha Ndapo wilayani Makete anayetuhumiwa kwa kosa la wizi wa
jumla ya Tshs 7,968,060/=
4.CC.15/2020 jamhuri dhidi ya Benson Anyingisye Mbwilo
mtendaji wa kijiji cha Ludodolelo wilayani Makete anayetuhumiwa kwa kosa
la wizi wa jumla ya Tshs 16,220,098/=
5.CC.16/2020 jamhuri dhidi ya Salim saleh Salim mtendaji wa
kijiji cha Kisinga wilayani Makete anayetuhumiwa kwa kosa la wizi wa
jumla ya Tshs 28,212,970/=
6.CC.17/2020 jamhuri dhidi ya Ebson Issa Mahenge mtendaji
wa kijiji cha Mbalache wilayani Makete anayetuhumiwa kwa wizi wa jumla
ya Tshs 14,350,160/=
7.CC.18/2020 jamhuri dhidi ya Victor Frank Mapunda mtendaji
wa kijiji cha Ilindwe wilayani Makete anayetuhumiwa kwa kosa la wizi wa
jumla Tshs 5,175,500/=
Na kufanya jumla ya kiasi cha fedha kilichoibwa na watumishi hao kupitia mashine za POS kuwa Tshs. 99,321,466/=.
Mukama amesema katika watuhumiwa hao jumla ya watuhumiwa
wanne ambao mashtaka yao yanazidi milioni 10 wamekosa dhamana kwa
kushidwa kutimiza masharti ya dhamana yaliyowekwa na mahakama hiyo ikiwa
ni pamoja na kuwe nusu ya fedha ambazo zinatuhumiwa kuibwa na
watuhumiwa hao ikiwa ni matakwa ya kisheria chini ya kifungu cha 148 (5)
(e) cha sheria ya mwenendo wa mashauri ya Jinai Sura ya 20 marejeo ya
mwaka 2002.
Aidha Mukama ametoa wito kwa watendaji wa vijiji,kata na
watu walioaminiwa na serikali kukusanya mapato ya halmashauri na
kuwasilisha kwa usahihi fedha zote katika akaunti za halmashauri .
Vile vile Takukuru mkoa wa Njombe inawataka wananchi na
watumishi wote wa umma kuwa wazalendo na kuungana na serikali katika
vita dhidi ya Rushwa ili kujenga na kukuza uchumi wa mko
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...