Na Amiri Kilagalila, Njombe

Jeshi la polisi mkoani Njombe limefanikiwa kukamata mtandao wa watu 23 wanaotuhumiwa kujihusisha na wizi wa mali mbalimbali yakiwemo magari matano,pikipiki 23 pamoja na vitu mbalimbali vya ndani zikiwemo tv.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Rashid Ngonyani mbele ya vyombo vya habari amesema ,kukamatwa kwa mali hizo kumekuja baada ya kufanyika kwa oparesheni mbalimbali za mitandao ya wizi.

“tunawashikilia watu 23 kwa makosa mbali mbali,watano kwa wizi wa magari,saba kwa wizi wa pikipiki na watuhumiwa 11 kwa makosa ya uvunjaji”alisema Ngonyani

Vile vile amesema jeshi hilo linashikilia gari aina ya Nadia na bajaji zinazotumika kubebea vitu ammbavyo vinapatikana kwa uvunjaji huku pia wakishikilia vipuli vya magali,kopyuta,laptop pamoja na TV 11 aina ya Flat screen.

Kamanda Ngonyani amesema miongoni mwa sababu ya kushikilia gari zilizo nyingi ni kutokana na utofauti wa namba za usajili,Chesisi pamoja na namba za Injini.

Aidha jeshi la polisi limetoa rai kwa wananchi kuacha kununua na kupokea mali za wizi kwa kuwa muda wowote zinaweza kuleta matatizo,huku jeshi hilo pia likiwataka waliobiwa mali hizo kufika kituo cha polisi na kutambua mali zao.

Justin Mnyalape ni mkazi wa mtaa wa Matalawe Sido ambaye tv yake iliyoibiwa takribani miezi minne iliyopita ni miongoni mwa mali zilizokamatwa ameshukuru jeshi la polisi kufanikisha ukamataji wa mali yake kwa kuwa alishakata tamaa.

“Jeshi limejipanga vizuri na ninatoa ushuhuda kwa kuwa ninona mali zangu zinaonekana na mimi nilikata tamaa,kwa mda mrefu tulikuwa tunaibiwa unakwenda kuandikisha polisi lakini mali haipatikani ila kwa sasa jeshi naamini kabisa linafanya kazi ipasavyo”alisem Mnyalape
Miongoni mwa mali za wizi zilizokamatwa na jeshi la polisi yakiwemo magari matano.
 Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Njombe, Rashid Ngonyani akizungumza na waandishi wa habari namna jeshi hilo lilivyofanikiwa kukamata mali za wizi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...