WAZIRI wa Maji,Profesa Makame Mbarawa akizungumza mara baada ya kupokeataarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji wakati wa ziara yake ya sikutatu mkoani Tanga iliyoanza leo kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly

Mkurugenziwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (TangaUwasa) Mhandisi Geofrey Hilly akizungumza wakati wa ziara hiyo kushotoni Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo

WAZIRIwa Maji,Profesa Makame Mbarawa kulia akinawa mikono kabla ya kuingiakwenye ukumbi wa mamlaka ya maji Safi na Usafi wa Mazingira JijiniTanga(Tanga Uwasa) wakati wa ziara yake
WAZIRI wa Maji,Profesa Makame Mbarawa kushoto akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi Mamlakaya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) MhandisiGeofrey Hillywakati wa ziara yake mara baada ya kutembelea chanzo chamaji eneo la Horohoro wilayani Mkinga katikati ni Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo

WAZIRI wa Maji,Profesa Makame Mbarawa kulia akiwa na Mkurugenzi Mamlaka
ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi
Geofrey Hilly wakati akitoka kutembelea miradi wa maji eneo la Horohoro

WAZIRI wa Maji,Profesa Makame Mbarawa akitoka kutembelea miradi wa maji eneo la Horohoro
WAZIRI wa Maji,Profesa Makame Mbarawaamemuondoa kwenye nafasi yake aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Menejimenti ya Manunuzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi waMazingira jijini Tanga(Tanga UWASA)Jamal Ngereja kwa kushindwa kufanya taratibuza manunuzi ya mabomba na vifaa katika miradi saba ya maji katika wilaya nnemkoani Tanga inayotekelezwa na Mamlaka hiyo.

Pia ProfesaMbarawa amefanya maamuzi hayo katika Mamlaka za Maji Safi na Usafi wa Mazingiraza Moshi,Babati na Arusha nakuahidi kuendelea kufanya mabadiliko katika mamlaka nyingine za maji zaMorogoro,Mwanza,Tabora,Shinyanga na Kahama.

ProfesaMbarawa amefikia uamuzi huo baada ya Wizara ya Maji kutoa fedha takribaniSh.Milioni 700 katika miradi saba ya maji katika wilaya zaPangani,Mkinga,Muheza na Handeni kwa ajili ya ununuzi wa mabomba tangu mweziNovemba mwaka jana lakini hakuna chochote kilichofanyika.

Pamoja na kufanya maamuzi hayo lakini pia aliwaonya wahasibu katika
mamlaka za maji nchini nao wajiandae iwapo tu watafanya uzembe katika matumizi ya fedha za miradi yamaji .“Haiwezekanitumetoa fedha za utekelezaji wa miradi ya maji katika mikoa ya Mbeya,Iringa naTanga kiasi hicho hicho cha fedha lakini wenzenu wamefikia asilimia 70 ya
utekelezaji lakini Tanga hakunakilichofanyika,”alisema.

Aliongeza,“ kutokana na hilo nakuambia kabisa wewe(Afisa Manunuzi) nakuondoa hapa na hilinitafanya pia kwenye mamlaka za MajiSafi na Usafi wa Mazingira za Morogoro,Mwanza,Kahama,Shinyanga na Tabora kama nilivyofanya Babati,Moshi na Arusha,”alisema.

Aidha,kwa upande wa miradi ya maji ambayo haiendi vizuri haswa ya mabwawa,ProfesaMbarawa aliahidi kuhakikisha anapeleka wataalamu kutoka wizarani kuchunguzamiradi hiyo kila kitu ilikujua kama inakwenda na thamani ya fedha zilizotumika.

“Nitahakikishakuwa ndani ya wiki kwenye miradi ya maji ambayo haiendi vizuri tunaletawataalamu kuja kuchunguza kila item(kitu)kuanzia tofali,urefu wa kibanda,kina cha mabwawa kuona kama inakwenda na valuefor money (thamani ya fedha),kutokana tumegundua kuna watu kuanzia ngazi yaHalmashauri hadi Wizarani walihusika nahujuma za miradi ya maji kwa kupandisha gharama,”alisema.

Aliongeza, “Nataka nimiambie wakandarasi nawatumishi wa Wizara ambao wamehusika nahuo mchezo mchafu wajiandae safari hii hatuna mchezo”.Katikahatua nyingine,Waziri Mbarawa amesema kuwa katika mwaka wa fedha2020/21,Serikali kupitia Wizara ya Maji imetenga fedha kwa ajili ya kutoa majikatika chanzo cha mto Zigi hadi katika mjiwa Horohoro wilayani Mkinga wenyeurefu wa kilometa 40.

Amesemakuwa,mradi huo utavinufaisha vijiji zaidi ya 30 vitakavyopitiwa na mradi huo nakuahidi pia kuleta wataalamu wa Wakala wa Uchimbaji Visima na Ujenzi(DDCA) kujakuchunguza na kufanya tathminikatika bwawa la maji la Horohoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...