Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MBUNGE wa Jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam Said Kubenea ameshauri ni kwanini misikiti na makanisa yasifungwe ili kuepusha waumini wa dini hizo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 (Corona).

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Kubenea amesema pamoja na hatua mbalimbali ambazo zinachukuliwa na Serikali na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto lakini iko haja ya kuchukua hatua zaidi ya zilizopo sasa.

Kubenea amesema kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani(WHO) ni kwamba katika wiki mbili zijazo hali itakuwa mbaya sana na kutakuwa na vifo vingi vya wagonjwa wa Corona.

Amesema kuwa kuna umuhimu  wa jamii kushiriki kikamilifu katika juhudi za kupambana na virusi vya Corona. Kwanini misikiti na makanisa yasifungwe kama hatua moja wapo ya kupunguza kasi ya kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa huu, makanisani na misikiti ni maeneo ambayo kunakuwa na idadi kubwa ya waumini , hivyo iko haja ya kufunga nyumba za ibada.

"Mimi ni Muislamu na tunafahamu kutokana na Corona ibada ya Hijja imefutwa kwa mwaka huu na huko ndiko ambako Mtume Muhammad (SAW) amezaliwa katika miji ya Makkah na Madina,
Ndugu zangu wa Kiislamu waache kwenda kwenye misiti ambako kuna mkunyasiko, Saudi Arabia ambako Mtume Mohhamad alikozaliwa wamefuta ibada ya Hijja, sisi huku nani?Hijja ni nguzo ya Tano kwenye Uislamu na bado imefutwa" ameeleza.

Pia amesema;"Vatcan wamefunga  makanisa ambako ndiko Papa Mtakatifu yupo na wamekubali kufunga makanisa.Hili gonjwa sio mchezo , ni vema hapa kwetu tukaacha kufanya mzaha mzaha,"ameseam Kubenea.

Ameongeza kuwa hiyo marufuku ya kupunguza msongamano wa watu kwenye maeneo mbalimbali itasaidia  katika kupunguza maambukizi na kwamba Tanzania sio kisiwa kiasi cha kuamini iko salama.

Kubenea pia amesema kuna haja ya Watanzania kuungana na kuhamasisha jamii kuchukua tahadhari ya ugonjwa huo hatari na dunia yote leo inalia.

Akizungumzia Jimbo lake la Ubungo jijini Dar es Salaam, Kubenea amesema kuwa jimbo lake liko hatarini zaidi kwa wananchi wake kupata maambukizi kutokana na muingiliano mkubwa wa watu kutoka eneo moja na jingine.

"Jimbo la Ubungo ambalo mimi ni Mbunge wake ni kitovu cha biashara , Ubungo ni eneo ambalo kuna muingiliano wa watu wa mikoa mbalimbali kwa kutumia Kituo cha Mabasi ya Mikoani Ubungo.

"Kuna watu ambao wanatoka nje ya nchi ili kwenda kwenye mikoa yao lazima wapite Ubungo.Pia watu wa maeneo mbalimbali ya ya Jiji la Dar es Salaam nao lazima wapite eneo hilo wanapokwenda mikoani, hivyo tupo kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi,"amesema Kubenea.

Pia amesema kuwa jana ameona picha kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha idadi ya watu walioko kwenye kituo cha mabasi ya Mwendokasi na kwa namna ya picha hizo ziaonesha wazi bado kunahitajika hatua zaidi kukabiliana na Corona.

"Pamoja na jitihada kubwa ambazo zinachukuliwa lakini kwa namna ambavyo hali inavyoonesha jitihada hizo zinapaswa kuungwa mkono na jamii kwa kufuata ushauri wa watu mbalimbali," amesema Kubenea.

Ameongeza kuwa Corona imeleta changamoto nyingi kwenye nchi nyingi duniani zikiwemo zenye uchumi mkubwa na uwezo katika kila kitu na bado wako kwenye matatizo.
"Nchi tajiri ambazo zimeatuacha mbali zinahangaika, sembuse sisi Tanzania, tukuchukue tahadhari na kuacha mzaha." Ameongeza.

Hata hivyo amempongeza Spika wa Bunge Job Ndugai kwa hatua ambazo amechukua kuhakikisha wabunge na wafanyakazi wa Bunge wanakuwa salama kwa kutopata maambukizi ya Corona lakini ameshauri  haja ya kutafakari na kuchukua hatua zaidi ya hapo.


MBUNGE wa Jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam Said Kubenea

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...