Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 08/04/2020 ofisini kwake jijini Dodoma ambapo ameitaka kampuni ya Benchmark 360 Ltd ambao ni waandaji wa mashindano ya kutafuta vipaji vya muziki ya Bongo Star Search (BSS) kumlipa mshindi wa mashindano ya BSS 2019 Ndg. Meshack Fukuta ndani ya mwezi mmoja kuanzia leo.

Meshack aliibuka mshindi kwenye mashindano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana ambapo kampuni ya Benchmark walitakiwa kumlipa mshindi kiasi cha shilingi milioni 50 ambapo kati ya hizo, milioni 30 ni kwa ajili ya usimamizi na promotion na milioni 20 alipaswa kukabidhiwa mkononi. Hata hivyo hadi kufikia leo Benchmark hawajamlipa Ndg. Meshack jambo lililopelekea kuleta malalamiko yake kwa Naibu Waziri.

Naibu Waziri amesisitiza kuwa endapo kampuni ya Benchmark haitokamilisha malipo hayo ndani ya mwezi mmoja basi hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuyafungia mashindano hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...