Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

 Wananchi waliojiandikisha katika Daftari la wapiga kura Mwaka 2015 na wale waliojiandikisha katika Uboreshaji wa Daftari Awamu ya kwanza wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuhakiki taarifa zao pindi Daftari litakapowekwa wazi katika maeneo yao na watumie njia nyingine za uhakiki Kama ilivyoelekezwa.

Rai imetolewa leo Jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa Semistocles Kaijage katika ufunguzi wa mkutano ulioandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na vyama vya siasa kwa ajili kuweka wazi mabadiliko yaliyojitojeza kwenye Daftari la Awamu ya Pili ya Kupigia kura na kukabidhi nakala Kwa wawakilishi wa vyama vya siasa

Jaji Kaijage amesema uboreshaji huo utaanza Aprili 17 na kukamilika Mei 4 mwaka huu kwa nchi nzima ambapo wamegawa katika ruti  tatu  na kufanyika kwa siku tatu kwa kila mkoa kwa Tanzania bara na Vusiwani.

Hata hivyo amesema kwa jumla ya vituo vitakavyotumika awamu hii ni 4006 badala ya 8031  vilivyokuwa vimekubaliwa hapo awali ambapo kwa sass vituo  3956  vitakuwa Tanzania bara na 50 Zanzibar.

Aidha amesema uboreshaji huu utafanyika katika kila Kata ambapo kutakuwa na Mwandishi Msaidizi na BVR kit Operator ambao watakuwa na orodha ya vituo vyote katika Kata husika na watendaji hao watakuwa na uwezo wa kuboresha taarifa za mpiga kura yeyote.

Aidha amesema wananchi hususani wenye sifa ya kujiandikisha kama wapiga kura wapya wasisubiri kujitokeza siku ya mwisho ya zoezi na hivyo kusababisha msongamano bali wafike vituoni mara tu zoezi litakapowafikia na watuze kadi zao.

Sambamba na hayo Jaji Kaijage amesema NEC haina wataalamu wa Afya ila imenunua vifaa vya kujikinga kwa ajili ya kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Covid 19 unaisababishwa na virusi vya corona  na tayari wametoa maelekezo kwa watendaji wake kuzingatia miongozo ya wataalamu wa Afya.
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Semistocles  Kaijage akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa nchini katika kuelekea Uchaguzi Mkuu  wa  Uboreshaji wa Daftari la Mipiga Kura awamu ya pili.
 Mkurugenzi wa Uchazi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt.Wilson Mahera akitoa akizungumza wakati wa kumkaribisha  Mwenyekiti wa Tume hiyo wakati wa Mkutano  vyama vya siasa wa Uboreshaji wa Daftari la Mipiga Kura awamu pili utaoanza hivi karibuni.
 Msajili wa vyama vya Siasa Jaji Mstaafu Francis Mutungi akiteta jambo na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya siasa nchini John Shibuda wakati Mkutano wa vyama vya Siasa na NEC.
 Naibu Katibu Mkuu wa Chama CHAUMA Eugene Kabendera akitoa akiuliza swali kuhusiana na uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mipiga Kura awamu ya pili katika Mkutano wa Vyama vya Siasa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

 Mkurugenzi wa Oparesheni na Mafunzo wa Chadema Benson Kigaila akichangia katika  katika Mkutano vya Siasa na NEC uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu  Semitocles Kaijage akijibu maswali ya viongozi wa vyama vya Siasa katika Mkutano wa Vyama hivyo na NEC  uliofanyika jijini Dar es Salaam.

 Mkutano ukiendelea  kati ya vyama vya Siasa na NEC

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...