Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii Forum Maxence Melo kulipa faini ya Sh. Milioni tatu ama kutumikia kifungo cha mwaka mmoja gerezani baada ya kupatikana na hatia katika kosa la kuzuia jeshi la polisi kufanya kazi yao ya uchunguzi kwa kuzuia taarifa binafsi za wateja wa mtandao wao.

Hukumu hiyo imesomwa leo Aprili 8,2020 na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba.

Hata hivyo mahakama imemuachia huru mshtakiwa Micke William ambaye ni Mwanahisa wa mtandao wa Jamii Forum,  baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake.
Mshtakiwa Maxence Mello ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa Kijamii wa Jamii Forum akipelekwa chini ya ulinzi baada ya Hakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumkuta na hatia katika kosa la kuzuia jeshi la polisi kufanya kazi yao ambapo amehukumiwa kulipa faini ya Sh. Milioni tatu ama kutumikia kifungo cha mwaka mmoja gerezani.

Mshtakiwa Maxence Melo wa kwanza kulia, Micke William  katikati na wakili wa kujitegeme Nashony Nkungu wakiwa wamesimama nje ya ukumbi wa mahakama ha Hakimu Mkazi Kisutu kabla ya kusomewa hukumu yao 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...