Charles James, Globu ya Jamii

KATIKA kukuza elimu na kuendana na sera ya elimu bila malipo, serikali imetoa mabati 324 kwa Shule ya Msingi Manungu iliyopo wilayani Kongwa mkoani Dodoma.

Akizungumza katika ziara yake ya kukagua miundombinu ya elimu wilayani humo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mwita Waitara amesema mabati hayo yatatumika kuezeka madarasa matano yaliyojengwa kwa nguvu za wananachi.

Waitara amesema serikali imefurahishwa na nguvu iliyotumika na wananchi hao chini ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Deo Ndejembi katika kuleta maendeleo kwenye sekta ya elimu.

" Niwapongeze wananchi wa Wilaya hii na hasa Mhe DC kwa kuwasimamia vema, kama serikali tumefurahishwa sana na juhudi zenu, hivyo ndani ya wiki mbili mabati hayo ya geji 28 yatatua hapa, ili kukamilisha ujenzi wa madarasa haya," Amesema Waitara.

Waitara amesema lengo la serikali ni kuona baada ya shule kufunguliwa endapo hali ya ugonjwa wa Corona itatengamaa basi ni kuona madarasa hayo yanakamilika ili yaweze kutumika.

Kwa upande wake DC Ndejembi ameahidi kuhakikish tunasimamia mabati hayo yaliyotoleww ili yatumike vizuri kama ilivyokusudiwa na vyumba hivyo vya madarasa vikamilike.

" Naibu Waziri kwa niaba ya wananchi wangu wa Kongwa tutoe shukrani zetu kwa serikali yetu inayoongozwa na jemedari wetu Rais Magufuli, mabati haya ni mengi sana kwetu na tunaahidi vyumba hivi vitano vitakamilike katika muda uliopangwa.

Hii ni motisha kwetu kuhakikisha tunapandisha kiwango chetu cha ufaulu kwa matokeo ya Darasa la saba na kidato cha nne ili kumpa zawadi Rais Magufuli ya kutupatia elimu bila malipo lakini pia kutuboreshea miundombinu yetu ya elimu, " Amesema Ndejembi.
 Muonekano wa Shule ya Manungu iliyopo wilayani Kongwa, Dodoma ambayo serikali imeahidi kutoa mabati 324 ndani ya wiki mbili.
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mwita Waitaa akizungumza na viongozi wa Wilaya ya Kongwa baada ya kufanya ziara ya kukagua miundombinu ya elimu wilayani humo.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mwita Waitara (kushoto) akikagua miundombinu ya elimu katika Wilaya Kongwa alipofanya ziara yake ya kikazi leo. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Deo Ndejembi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...