Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, Giles Muroto akionesha kwa wandishi wa habari bastola aina ya browning no.016975 ambayo wameikamata kwa kijana ambaye alikua akiimiliki kimakosa na kuitumia kufanyia uhalifu.
Charles James, Michuzi TV
ASKARI wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) amesaidia kumkamata kijana mmoja jijini Dodoma akiwa na silaha Bastola aina ya browning yenye no.016975 akimiliki kinyume na sheria huku akiitumia kufanyia uhalifu.

Akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Giles Muroto amesema kijana huyo tayari anashikiliwa na Polisi na muda wowote atafikishwa mahakamani.

" Tunamshukuru sana askari huyu wa JWTZ hii ni kuonesha jinsi gani majeshi yetu haya yamekua yakishirikiana kwa karibu katika kutokomeza uhalifu, kulinda usalama wa raia na mali zake, tutoe wito pia kwa wananchi wetu kutoa taarifa pindi wanapoona uhalifu kwenye maeneo yao," Amesema Muroto.

Akizungumzia wizi wa magari unaondelea mkoani Dodoma, Kamanda Muroto amesema wezi wote wanaohusika na wizi huo wajisalimishe na kurudisha magari ya watu na kwamba siku zao zinahesabika.

Amewataka wananchi wa Dodoma na wote wanaochukia uhalifu kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha wanadhibiti huo ambao mpaka sasa magari matano yameshaibiwa.

" Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma tunaomba wananchi kuwa watulivu wakati huu ambao tunafanya kazi ya kuwabaini wahalifu hao, uvumilivu unahitaji na tuwe na imani na vyombo vyetu siku za wezi hao zinahesabika.

Nitoe rai kwa wananchi kuchukua tahadhari zote ikiwemo kufunga car track systems kwenye magari yao au camera ili kuongeza utambuzi wa wahalifu hao, wenye magari wawe makini na waosha magari na mafundi wao," Amesema Muroto.

Kamanda Muroto pia amewataka wauza spea na vipuri vya magari au vyuma chakavu wanaopokea kwa watu wajiridhishe na uhalali wake na namna vilivyopatikana, pia wasisafirishe kwenda maeneo mengine pasipokukaguliwa na Polisi.

Amesema wenye gereji bubu lazima wafichuliwe kwa kuwa ni vivutio vya wahalifu kujificha na kukata vipuli vya magari na kuwataka wananchi wawafichue waweze kupekuliwa na kuchunguzwa na wote wanaomiliki magari yasiyo halali wajisalimishe kituo cha Polisi.
 Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, Giles Muroto akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...