Na Jumbe Ismailly SINGIDA

MKUU wa Mkoa wa Singida,Dkt Rehema Nchimbi amesema serikali Mkoani hapa inatarajia kuwafungia watu wote wanaofanya biashara za kuuza pombe za asili (kienyeji) watakaoshindwa kutekeleza maagizo ya kujikinga na ugonjwa wa korona.

Dkt Nchimbi alitoa agizo hilo kwenye mkutano wa Baraza la Jumuiya wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Singida waliokutana kujadiliana pamoja na mambo mengine tahadhari ya kujikinga na janga na kitaifa la ugonjwa hata korona.

Mkuu huyo wa Mkoa ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya afya ya Mkoa huo alisema katika kipindi hiki kigumu wauzaji wa pombe hiyo watatakiwa kuhakikisha kila mteja wanayemuhudumia anakuwa na chombo chake cha kuwekewa kinywaji hicho,tofauti na ilivyozoeleka kwa kunywa pombe hiyo kwa kuchangia chombo kimoja.

“Kila mmoja anayetaka kufanya biashara hiyo ni lazima ahakikishe kwamba kila mmoja ananawa mikono yake kwa kutumia maji yanayotiririka na sabuni,kukaa mbali mbali,ni lazima kila mmoja awe na chombo chake hatuoni vibaya kama kila mtu atakuja na chungu sawa,atakuja na kopo haya na akija na sijui na kitu gani haya au hata akikutana na chupa akaikata sa cha msingi ni kila mtu awe na chombo chake.:”alisisitiza Dkt Nchimbi.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa huyo kazi ya muuzaji itakauwa ni kuwachotea pombe hiyo na siyo kila mtu kuingia kwenye chombo kilichohifadhiwa pombe na kuanza kujichotea bali ni yule tu aliyeweka kinga na kitakasa mikono na siyo vinginevyo.

Dkt Nchimbi ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa Mkoa aliagiza pia kwamba mfanyabiashara yeyote yule ambaye hataweza kutekeleza maagaizo hayo hawatasita kumfungia biashara yake na kwamba kabla ya kuruhusu biashara hiyo kutafanyika ukaguzi kwa wanaojihusisha na biashara hiyo ndipo waweze kuruhusiwa.

Aidha kiongozi huyo wa Mkoa hata hivyo alifafanua kuwa hapatakuwa na ruhusa kwa wanywaji wa kinywaji hicho kupokezana kama mbio za vijijiti na atakayetimiza masharti hayo ataruhusiwa kiungwana,kiutu na hayo ndiyo maagizo na msimamo wa Mkoa.

Kuhusu tahadhari kwa watumiaji wa pombe hizo watakaoonekana kuwa wameshalewa,Mkuu wa Mkoa alisisitiza kuwa atafukuzwa kwenye duka la kuuzia pombe hiyo kwani sababu mlevi hawezi kuzingatia tena masharti ya karantini ya ugonjwa huo,kuna uwezekano wa kuanza kumwagamwaga pombe na hata kuwakumbatia wengine.

“Mgambo au jeshi la akaiba watakuwepo imara wakiona tu dalili za hali ya kuzidiwa na kinywaji wanakutoa na akifanya upuuzi wa kutotii tunamchukulia hatua za kisheria,na hivyo na hivyo ndivyo angalizo letu kwa watumiaji wa kinywaji hicho.”alisisitiza.

Kwa upande wao baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wa UWT Mkoa wa Singida waliishauri serikali kuangalia uwezekano wa kuendelea kutoa elimu kwenye maeneo ya vijijini ambako kwa kiasi kikubwa bado elimu hiyo haijawafikia wananhi kwenye maeneo hayo.

Akionyesha hofu yake juu ya tahadhari kwa wanywaji wa pombe za asili,Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Masnyoni,Blandina Mawala alisema akiwa katika ziara zake wilayani kwake alishuhudia wanywaji wa pombe hiyo licha ya kunawa maji,lakini wamekuwa wakichangia chombo kimoja kunywa pombe hiyo.

“Jamani elimu hii vijijini haipo mimi nimetembelea kijiji fulani juzi tu lakini ni kweli yule mama mwuza anayeuza pombe zile za kienyeji ameweka maji kkweli pale wananawa,lakini wakishanawa wanakuja kunywa zile pombe za lita wapo kama watano au saba lakini wamenawa mikono sijui sasa usalamawao pale ukoje.?alihoji mwenyekiti huyo kuonyesha hofu ya kuenea kwa gonjwa hilo wiulayani kwao.

Naye Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Singida,Jenny Efraimu Kessy alisisitiza kwamba korona ni ugonjwa hatari sana na kuwashauri kuwa kila mfanyabiashara ahakikishe wateja wake wananawa maji na sabuni kwanza kabla ya kuingia na kununua biadhaa wanazohitaji.

“Jamani mwenzenu kuna wafanyabiashara kama wanne hivi tunaofanyanao biashara kutoka China,lakini nawatafuta kwenye simu siwapati wote wameshakufa,huu ni ugonjwa hatari sana ndugu zangu ila hali ni mbaya tucheke tu hapa twendeni tukatoe elimu hii kwenye wilaya zetu.”alifafanua Kessy.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dkt.Rehema Nchimbi(wa kwanza kutoka kulia) akifungua mkutano wa baraza la UWT Mkoa wa Singida lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM Mkoa wa Singida.(Picha zote Na Jumbe Ismailly).
 Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dkt Rehema Nchimbi (wa kwanza kutoka kulia),Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Singida,Jenny Kessy(wa pili kutoka kushoto) wakiwa na Katibu wa UWT Mkoa wa Singida wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya mkutano wa Baraza la UWT mkoa kuanza.
 Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Singida,Jenny Kessy(wa pili kutpoka kushoto) akiteta jambo na Katibu wa UWT Mkoa wa Singida wakati wa mkutano wa baraza la uwt mkoa lililofanyikaq kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM Mkoa wa Singida.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...