TAASISI
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoani Manyara, imewasaidia
wamiliki wa migodi 14 wa madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani
Wilayani Simanjiro waliokuwa wafutiwe leseni zao kwa kudaiwa shilingi
milioni 14.5 na Wizara ya Madini.
Kwa
mujibu wa Mkuu wa Takukuru mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu
wamiliki hao 14 wa migodi walikuwa wanyang'anywe migodi hiyo kwa
kutolipa ada za leseni zao.
Alisema Takukuru wilaya ya Simanjiro iliingilia kati katika kudai fedha hizo ambapo ilikusanya shilingi milioni 19 na kufungua akaunti maalum ili zikikamilika zikabidhiwe kwenye chama hicho cha ushirika.
Alisema Takukuru wilaya ya Simanjiro iliingilia kati katika kudai fedha hizo ambapo ilikusanya shilingi milioni 19 na kufungua akaunti maalum ili zikikamilika zikabidhiwe kwenye chama hicho cha ushirika.
Makungu
alisema leseni hizo zilizopo kitalu B (Opec) zilikuwa zifutwe kwa
wanachama hao wa chama cha ushirika cha Mirerani and Naisinyai Small
Miners Primary Cooperative Society (Minasco) waliokuwa wanadaiwa fedha
hizo.
Alisema awali
chama hicho chenye wanachama 50 kilikuwa kinawadai baadhi ya wanachama
wake shilingi milioni 58 tangu mwaka 2018, ambayo ni asilimia tano ya
mapato ya madini.
"Huu
ni utekelezaji wa maagizo ya Rais John Magufuli ya kusimamia urejeshaji
wa fedha za vyama vya ushirika sasa miongoni mwa vyama hivyo ni hii
Minasco ambayo tuliingilia kati na kufanikisha upatikanaji wa fedha
hizo," alisema.
Alisema
baada ya kupata taarifa kwa mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika wa
Manyara ya wachimbaji hao kudaiwa shilingi milioni 14.5 za ada za leseni
waliingilia kati ili kuwanusuru ili wasifutiwe leseni.
Alisema
kutokana na mazingira hayo waliona ni busara kuwakabidhi fedha hizo na
kusimamia kuhakikisha zinakwenda kulipa deni la leseni ili wachimbaji
hao wadogo waendelee kufanya kazi shughuli zao za kila siku" alisema
Makungu.
Alisema endapo
Takukuru wasingeingilia kati na kusimamia urejeshwaji wa fedha hizo
leseni za wachimbaji hao zingefutwa na wengi wao wangekosa ajira.
Alitoa
wito kwa uongozi wa Minasco kusimamia mchango wa vyanzo vya mapato kwa
umakini na kuhakikisha fedha zisikae mikononi mwa watu binafsi bila
sababu za msingi na kuwa na mfumo thabiti wa ulipwaji fedha zao.
Alisema
kwa wanachama wa vyama vya ushirika wakiwemo Minasco wahakikishe
wanafanya wajibu wao kwa chama, wahakikishe wanafanya marejesho kwa
wakati, wahakikishe wanaandaa mfumo mzuri wa kuhifadhi fedha za chama
kwani siyo shamba la bibi.
Wachimbaji madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani
Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, ambapo Takukuru imefanikisha migodi
14 isifutiwe leseni kwa kuhakikisha shilingi milioni 14.5 zinalipiwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...