Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri yaTandahimba Said Msomoka ametoa eneo kwa ajili uwekezaji wa kiwanda na ghala la kisasa

Ameyasema hayo leo ofisini kwake wakati na kueleza kuwa kiwanda na ghala zitaleta tija kwa wakulima wa korosho ndani ya Wilaya

"Tunatoa eneo kwa ajili ya mtandao wa kijani kibichi Tanzania(Mkikita) ambao wanahitajibkujenga kiwanda na ghala,hivyo sisi Kama halmashauri tunawakaribisha kwakuwa maeneo yapo kwa ajili ya uwekezaji," amesema Msomoka

Naye mkurugenzi wa Mtandao wa Kijani kijichi Tanzania (Mkikita)Adam Ngamange  amesema kiwanda na ghala zinalenga kuipa thamani zao la korosho ya Tandahimba kuendelea kuwa Bora

" Tunahitaji kujenga kiwanda na ghala ,pia kliniki ya kilimo ambayo itahusika  kutoa mafunzo ya kilimo,ushauri wa kilimo,mtaji na pembejeo kwa wakulima wa korosho,"amesema Ngamange.
 Mkurugenzi wa Mkikita alitembelea kiwanda kidogo Cha kubangua korosho Tandahimba
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Said Msomoka akiwa na Mkurugenzi wa Mkikita Adam Ngamange.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Saidi Msomoka (kushoto)akiwa na Mkurugenzi wa Mkikita Adam Ngamange na viongozi wengine wa wakulima .
 

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...