Mwandishi wa Habari wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd inayochapisha Magazeti ya Mtanzania,Rai, Bingwa na Dimba pamoja na Mtanzania Digital bwana Eliya Mbonea amefariki dunia leo Jumatatu Aprili 6,2020 wakati akiendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari mkoa wa Arusha (Arusha Press Club), Claude Gwandu amethibitisha taarifa za kifo cha Eliya Mbonea alipozungumza na Malunde 1 blog mchana huu.

"Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha(APC) kinasikitika kutangaza kifo cha mwanachama wake,Eliya Mbonea kilichotokea alasiri ya leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili",amesema Gwandu.

Amesema Mbonea ambaye pia alikuwa Katibu Mkuu wa APC kuanzia 2010 hadi 2013 alihamishiwa Muhimbili wiki tatu zilizopita kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda KCMC mjini Moshi ambako alikuwa akipatIwa matibabu tangu Februari 19, mwaka huu.

"Mwili wa marehemu unatarajiwa kuzikwa Arusha na taarifa zaidi zitatolewa baada ya kukutana na familia yake baadaye  leo jioni",amesema Gwandu.

Mungu Ailaze Mahali Pema Peponi Roho ya Marehemu Eliya Mbonea. Amina

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...