Na Said Mwishehe, Michuzi TV

KATIKA kuepuka mikusanyiko kama sehemu ya kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa COVID-19(Corona) , Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)umeamua kuadhimisha kilele cha siku ya upandaji miti kitaifa kwa kugawa miche ya miti kwa wananchi.

TFS imegawa miche hiyo ya miti ya aina mbalimbali leo Aprili 1, mwaka 2020 jijini Dar es Salaam huku ikitoa rai kwa wananchi wa Dar es Salaam,Tanga na Pwani kutumia kipindi hiki cha mvua za masika kupanda miti kwa wingi.

Akizungumza wakati wa ugawaji huo wa miche ya miti uliofanyika katika Ofisi za TFS zilizopo Jengo la Mpingo Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Misitu na Ufugaji Nyuki wa Wakala huo Zawadi Mbwambo amesema kwa mwaka huu maadhimisho ya siku ya upandaji miti yalikuwa yafanyike kitaifa mkoani Mtwara lakini wameamua kila kanda igawe miche ya miti kwa wananchi.

Amefafanua katika kilele cha siku ya kupanda miti huwa kunakuwa na wageni waalikwa wakiwemo viongozi kutoka Serikali na wadau wengine wa misitu na hivyo hukusanya watu wengi, hivyo katika kujali afya za Watanzania, TFS imeamua badala ya kukusanyika sehemu moja ni vema wakatumia kilele hicho kugawa miche ya miti kwa wananchi kama sehemu mojawapo ya kuepuka mkusanyiko.

"Kila ifikapo Aprili Mosi ya kila mwaka TFS tumekuwa tukihamasisha upandaji miti.Leo tunatumia nafasi hii pamoja na kuhamasisha upandaji miti lakini tuaomba wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kwa kufuata maelekezo ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto kuhusu kujiepusha na virusi vya Corona,"amesema Mbwambo.

Kuhusu miche ya miti ambayo wameigawa kwa wananchi na kwa watumishi wa TFS, Mbwambo ameseme kwa siku ya leo wamegawa miche ya miti zaidi ya 300 na kwamba hiki ni kipindi ni kizuri kwa kupanda miti kwani ndio msimu wa mvua za masika.Hata hivyo kwa Dar es Salaam kuna zaidi ya miche 500,000 ambayo inasubiria wananchi wenye kuihitaji.

Ametumia nafasi hiyo kuhamasisha wananchi kupanda miti ya matunda kwani inafaida mbili ikiwemo ya kupata matunda na wakati huo huo unapata kivuli huku akifafanua miti ya matunda inachukua sehemu ndogo, hivyo hata wenye maeneo madogo ni rahisi kuipanda na kumea vizuri.
"TFS tunazo kanda saba na kote huko kuna miche ya miti ya kutosha ambayo inatolewa bure.Hata hivyo safari hii tumeamua wote ambao tunawapa miche ya miti tunaandika majina yao na namba zao za simu kwa ajili ya kufuatilia, kwani tumebaini wengi wanachukua miche lakini wanashindwa kuitunza,"amesema Mbwambo.

Kwa upande wa wananchia ambao wamepata miche ya miti hiyo uliyokuwa ikitolewa bure na TFS, wamesema kuwa wamefurahishwa na kitendo hicho na kwamba ni vema wananchi wakajitokeza kwenye ofisi za TFS kwa ajili ya kuchukua miche ya miti na kwenda kupanda katika maeneo yao.
Wamesema wanafahamu umuhimuwa miti na ndio mana waliposikia ikitangazwa miche ya miti inatolewa bure wakaichangamkia.

Shamari Jumanne ambaye ni moja ya wakazi wa Dar es Salaam waliopata miti hiyo amesema ili kuna umuhimu mkubwa kwa jamii kuendelea kupanda miti kwani inasaidia kupata hewa safi lakini pia uwepo wa miti kunasaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchia ambayo moya ya chanzo chake ni uharibifu wa mazingira na hasa kukata miti hivyo.

Kwa upande wake Meneja Mawasiliano wa TFS Martha Chassama amesema pia kwa upande wa Wilaya ya Kigamboni nako imetolewa miche 300 kwa wananchi.

"Mbali ya hii miche ya miti ambayo tumeigawa hapa ofisini kwetu, wilayani Kigamboni nako kuna miche ya miti imekwenda huko kwa ajili ya kugawa kwa wananchi,"amesema Chassama.
 :Mmoja wa wakazi wa jijini Dar es Salaam(kulia) akipokea miche ya miti kutoka kwa Mtumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho  ya Siku ya upandaji miti kitaifa yaliyofanyika leo Aprili Mosi mwaka 2020.
Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) wakiendelea kupanga miche ya miti kabla ya kuanza kuigawa kwa wananchi mbalimbali jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya upandaji miti kitaifa.
 Wakazi wa Dar es Salaam wakiwa kwenye ofisi za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) wakiendelea kuchukua miche
Baadhi ya wananchi wa Jiji la Dar es Salaam wakiendelea kupatiwa miche ya miti kwa ajili ya kwenda kuipanda katika maeneo yao wakati wa siku ya maadhimisho ya Siku ya upandaji mitikitaifa.
 Moja ya gari iliyobeba miche ya miti ikiwa kwenye ofisi za TFS jijini Dar es Salaam.Miche hiyo ya miti imegawiwa kwa wakazi wa jiji hilo kama sehemu ya kuadhimishi Siku ya upandaji miti kitaifa ambayo hufanyika ifikapo Aprili Mosi ya kila mwaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...