Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Adam Fimbo (kulia) akimkabidhi michoro ya ujenzi wa jengo la ofisi za TMDA Jijini Dodoma, Mhandisi Haikamen Mlekio wa NHC. Ujenzi wa ofisi hiyo unatarajiwa kuchukua miezi 12 toka tarehe 18 Aprili 2020 utakamilika tarehe 17 Aprili 2021

NA MWANDISHI WETU DODOMA.

MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TMDA) inatarajia kuanza ujenzi wa jengo la ofisi yake kanda ya Kati Dodoma, ujenzi huo unatarajia kuchukua miezi 12, toka18 Aprili 2020 na kutarajia kukamilika 17 Aprili 2021.

Akikabidhi michoro ya ujenzi wa jengo hilo litakalojengwa eneo la Ilazo jijini Dodoma, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Adam Fimbo kwa Mkandarasi wa Shirika la Nyumba (NHC), Injinia Haikamen Mlekio alieleza kuwa:

Kukamilika kwa ujenzi huu kutaiwezesha TMDA kutekeleza majukumu yake kiufanisi katika kuhudumia mikoa ya Kanda ya kati ambayo inajumuisha Dodoma, singida na Morogoro.

Hafla hiyo pia ilishuhudiwa na mtaalam Mshauri toka Chuo cha Ardhi, Bi. Neema Mbwambo na wadau wengine wakiwemo wafanyakazi wa TMDA.

TMDA ambayo hapo awali ilijulikana kama TFDA ni taasisi ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yenye jukumu la kusimamia ubora, usalama na ufanisi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi.

Lengo la taasisi hii ni kulinda afya ya Jamii dhidi ya madhara yanayoweza kutokea baada ya matumizi ya bidhaa husika.
Hafla ya makabidhiano ya michoro katika kiwanja cha TMDA yalishuhudiwa na Mtaalam Mshauri toka Ardhi University Bi. Neema Mbwambo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...