Umoja wa wazalishaji sabuni wadogo Tanzania (UWASWATA) unatarajia  kuungana na serikali katika mapambano  Virusi vya Corona kwa kutoa mchango wao wa Sabuni kwa ajili ya Hospitali Jijini Dar es Salaam.

Sabuni hizo zitatolewa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambaye atatoa sabuni hizo kutokana na uhitaji wa hospitali.

Akizungumza na Michuzi  TV Katibu wa Umoja huo Maria Lucas amesema kuwa hawawezi kuiachia serikali peke yake katika mapambano ya Virusi vya Corona.

Amesema Wana sabuni za aina mbalimbali zikiwemo za usafi   katika  hospitali.

Katibu anasema sabuni hizi zitapelekwa kwa mkuu wa mkoa kisha mkuu wa mkoa atatusaidia kuzigawa katika  hospitali  husika
Sabuni hizi zimezaslishwa na viwanda vidogo vya hapa nchini.

 Uwaswata ukisimamiwa na sido pamoja na ofisi ya Maamlaka yq  Maabara ya  Mkemia Mkuu  Serikali .

Amesema Tanzania ina viwanda vidogo ambavyo vinazslisha sabuni za Usafi wa mazingira na mwili pia tunazalisha vitakasa mikono mfano sanitizer pamoja na Sabuni ya Kunawia mikono.

"Sisi kama uwaswata tumeona ni vyema kuisaidia serikali yetu kwa kutoa sabuni zitakakwenda kusafisha mazingira ya hospitali zote za mkoa wa Dar es Salaam"amesema Lucas.

Lucas amesema wanaamini myUsafi daima kwa maendeleo ya nchi  na uchumi kwa wazawa kuitikia serikali ya awamu ya Tano ya Tanzania ya Viwanda.


Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...