Mwenyekiti wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Abdulla Makame akizungumza mara baada ya wabunge wa bunge la Afrika Mashariki kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wametembelea mpaka wa Kenya na Tanzania eneo la Horohoro –Lungalunga kuangalia umeathirika vipi kutokana na janga la Virusi vya Corona na hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa kuweza kukabiliana nao huku wakiridhishwa na hatua zinazochukuliwa kulia ni Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure
Mwenyekiti wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Jamhuri ya Muungano waTanzania Dkt Abdulla Makame akisisitiza jambo wakati walipotembeleampaka wa Kenya na Tanzania eneo la Horohoro ikiwemo upande wa pili wanchi ya Kenya
Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure akifuatilia jambo wakati wa ziara hiyo

Sehemu ya watumishi wa TRA mkoa wa Tanga wakifuatilia matukio mbalimbali
Mwenyekitiwa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Abdulla Makame kushoto akisalimiana na Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure wakati walipoingia kwenye Kituo cha Forodha Horohoro
WABUNGE wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Abdulla Makame na Mhandisi Mohamed Habibu Mnyaa

  WABUNGE wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Abdulla Makame na Mhandisi Mohamed Habibu Mnyaa katikati wakiangalia bidhaa mbalimbali mpakani hapo
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhandisi Mohamed Habibu Mnyaa katikati akinawa na santize kabla ya kuingia kwenye ofisi mbalimbali zilizopo mpakani hapo.

Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure kulia akiwa na Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Abdulla Makame wakitoka nje mara baada ya kufanya ziara yao



Wakipata picha ya pamoja mara baada ya kutembelea eneo hilo

Wakiwa kwenye picha ya pamoja na Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki

WABUNGE wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wametembelea mpaka wa Kenya na Tanzania eneo la Horohoro –Lungalunga kuangalia umeathirika vipi kutokana na janga la Virusi vya Corona na hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa kuweza kukabiliana nao huku wakiridhishwa na hatua zinazochukuliwa.

Mpaka wa Horohoro upo wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga na Kenya ambao umekuwa ukitumiwa na wananchi wa nchi hizo mbili kuweza kuvuka upande mmoja hadi mwengine lakini hivi sasa inaelezwa huwezi kuvuka bila kuwekwa chini ya uangalizi
kwa kipindi cha siku 14.

Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo hilo hivi karibuni Mwenyekiti wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Abdulla Makame ambayo pia walikuwa wameambatana na Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure huku akizipongeza mamlaka zilizopo mpakani hapo kutokana na hatua inazochukua
kukabiliana na janga hilo lakini kwa kuzingatia taratibu zilizotolewa
na Serikali.

Mwenyekiti huyo pia aliwapongeza watumishi
wanaofanya kazi kwenye sekta ya afya nchini kutokana na kuwa mstari wa
mbele kutoa huduma ikiwemo kuweka maisha yao rehani kuhakikihs
wanatuokoa na janga hilo hatari ambalo limekuwa tishio kubwa duniani.

Aidha alisema mpaka sasa nchi haijafunga mipaka yake na watu wanaendeela kuvuka lakini kwa tahadhari ya afya wanaovuka wataendelea kuwekwa chini ya uangalizi kwa siku 14 ili waweze kujiridhika kama ana maambukizi au la .

“Mpaka sasa hapa kwetu nchi haijafunga mipaka yake sababu
serikali inataka bidhaa muhimu ikiwemo vifaa tiba kwa kipindi hiki
vinahitajika vitaendelea kuvuka lakini watu wanaovuka watakwenda
karatini”Alisema Dkt Abdulla.

Mwenyekiti huyo alisema kwamba sio
kwamba watu wanazuiwa ili waonewe wanachoifanya ni kupambana na janga
la kitaifa ambalo limefanya mataifa makubwa watu wanalia, wanakufa hali
ni hatari na lazima hatua hizo zichukuliwe.

“Lakini pia
tumeambiwa hapa kwamba abiria wakivuka wanakaa karantine siku 14 katika
uangalizi kabla ya kuvuka tumeonyeshwaa maeneo na mengine tumeambiwea
yapo Tanga mjini kabla ya kuendelea na safari zao hilo zoezi lilikuwa ni
kuangalia abiria”Alisema

“Madereva walikuwa na utaratibu
tofauti kwa sababu wanapeleka mizigo na walisema hawataki mizigo isivuke
kutokana na baadhi yake ni vifaa ikiwemo tiba na vyakula ambavyo
vinahitajika kila siku na kuweka maisha yakawe sawasawa “Alisema

Mwenyekiti
huyo alisema kwamba lakini waraka namba 2 umetoka na kwa sasa madereva
nao watakuwa wakikaa karantine huo waraka utaanza kutekeleza kutokana na
hilo wameona maelekezo yanazidi kuwa makali lakini pamoja na ukali
wanasema mipaka bado ipo wazi na bidhaa muhimu zitaendelea kuvuka.

Hata
hivyo alisema watatumia utaratibu mwengine kwamba ama gari zishushe
mizigo mipakani ipandishwe magari mengine au gari ije ibadilishe
madereva mipakani na kuwekwa dawa na madereva kubaki kwenye nchi zao.


“Kimsingi maelekezo ya serikali yanaendelea kufuatwa na mpaka sasa
kwenye mpaka huo hajapatikana mgonjwa yoyote wa Corona lakini tumeambiwa wapo karatine watu 47 na watu wanne walishukiwa kuonyesha dalili
walipimwa wakawa hawana na waliruhusiwa”Alisema

Awali akizungumza kwa upande wake Mbunge mwengine wa Bunge hilo Mhandisi Mohamed Habibu Mnyaa alisema wamefika eneo hilo kwa lengo la kuona uelewa upo kiasi gani na taratibu zilizotangazwa na serikali za
kujilinda na virusi vya Corona umeeleweka kiasi gani na watu wanayafuata
kwa kiasi gani.

Alisema wao kama wabunge wa Bunge la Afrika
Mashariki wamelazimika wote kufanya kazi ndani ya nchi zao kushirikiana
na serikali na wananchi kuhusu kupiga vita maradhi ya virusi vya Corona
kwa hiyoi kwa upande wa Tanzania wamegawana vikundi vya watu wawili
wawili maeneo mengine mmoja kutembelea mipaka mbalimbali iliyopo nchini lengo kusaidia uelewa wa wananchi kupiga vita maradhi hayo.

Naye kwa upande wake Afisa Afya Mfawidhi Huruma Kimaro alisema katika mpaka huo hakuna mtu yoyote anayepita na wanaofika hapo wanapelekwa karatini na mpaka sasa watu 47 wapo karatine huku akieleza kwamba walipata washukiwa wanne walipopelekwa maabara walikuwa hawajaambukizwa waliwaruhusu na kuwapa maelekezo ikiwemo kutoa ushauri kwao kwa kuendelea kuwa mabalozi wazuri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...