Wafanyakazi wa hotel ya Naura Springs na Impala hotel pichani wanaodai mishahara yao 
Wafanyakazi wa Hotel za Impala na Naura Springs wanasotea mishahara yao tokea Mwezi wa Tisa mwaka jana huku uongozi wa kampuni hizo ukidai kuwa hauna fedha kutokana na Ugonjwa wa Covid 19.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wafanyakazi hao ambao wapo majumbani na wengine kazini  wakisotea mishahara yao bila kulipwa kwa zaidi ya miezi nane huku Mkurugenzi mbele ya waziri akiahidi kuwapa mishahara yao January 31 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Naibu waziri wa kazi ajira na watu wenye ulemavu Anthony Mavunde kwenye kikao chake na wafanyakazi wa hotel hizo na Mkurugenzi wao Randle Mrema walikubaliana kuanza malipo mnamo Mwezi wa January 2020 jambo.ambalo halijatekelezwa hadi leo hii.


"Ndugu mwandishi sisi tunaishi maisha ya kuomba omba wakati tuna mikataba ya kazi huku kwenye majumba tuliopanga tunadaiwa Kodi huku wengine wakiwa wamefukuzwa katika majumba hayo wengie ni wagonjwa hawajui kesho yao kutokana na kukosa malipo hayo aliyoahidi Mkurugenzi wetu  mbele ya waziri wa kazi kuwa atatulipa kila mwezi kama kawaida"alisema Sia Lyimo


Kwa Upande wake Kiongozi wa wafanyakazi hao wa Impala group  Lyimo alisema kuwa yeye amekuwa akipata lawama nyingi kutoka kwa wafanyakazi wenzake baada ya makubaliano ya awali mbele ya waziri kutotekelezwa hadi sasa Jambo linalowawia vigumu kujua hatma yao ni ipi.

Kwa mujibu wa wafanyakazi hao wanaodai malimbikizo ya mishahara ya miezi nane Sasa wamemuomba Rais na Serikali yake kuingilia kati sakata hilo ili waweze kupata haki na stahili zao kwani viongozi wa Serikali mkoa na wilaya wameshindwa kuwatendea haki kupata haki zetu huku tukiwa na mashaka nao.

Kwa nyakati tofauti huko nyuma Mkurugenzi wa Impala group of Companies Randle Mrema amekuwa akidai kampuni hiyo ikiwa kwenye hali mbaya ya kifedha na watajitahidi kuwalipa fedha zao ndani ya muda Jambo ambalo ameshindwa kulifanya.

Alipotafutwa kwa njia ya simu kujibu tuhuma hizo Randle Mrema simu yake haikupatikana kwa wakati wote na Juhudi zinaendelea ili kuweza kujibu tuhuma hizo za kushindwa kuwalipa mishahara kwa miezi minane Sasa.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...