Na Farida Saidy Morogoro
WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani amefanya ziara katika mradi wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme wa JULIUS NYERERE MW 2115 ambapo amekagua maeneo mbalimbali katika mradi huo na kuridhishwa na kazi inayofanywa na mkandarasi kwa hatua aliyofikia. 

Aidha Dkt Kalemani amemtaka mkandarasi wa mradi huo kuhakikisha anakarabati barabara zote za nje na ndani ya mradi ambazo zinatumika kupitisha mizigo inayoenda kwenye mradi,sambamba na kumtaka mkandarasi huyo kumaliza kazi kwa muda uliopangwa.

Kwa upande wake  Mkurugenzi wa shirika la umeme Tanzania TANESCO Tito Mwinuka na msimamizi wa mradi Mhandisi Steven Manda wamewahakikishia watanzania kuwa mradi huo utakamilika kwa wakati,hivyo wasiwe na shaka, kwani ukikamilika kwa mradi huo utakuza uchumi wao na Taifa kwa ujumla.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akitekeleza agizo la Serikali kupitia Wizara ya afya la kunawa mikono kwa sabauni na maji tiririka ili kupaamba na kuenea kwa virus covid 19 vinavyosababisha homa kali ya mapafu,kabla ya kuingia katika mradi wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme wa JULIUS NYERERE MW 2115 jana April 5, 2020.
 Msimamizi wa mradi wa kufua umeme wa JULIUS NYERERE MW 2115 Mhandisi Steven Manda akiongea na waandishi wa habari wakati wa ziara ya waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani  alipokwenda kutembelea maradi huo.
 Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua miundo mbinu ya mradi  wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme wa JULIUS NYERERE MW 2115 ambapo amelidhishwa na maendeleo ya mradi  huo
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akipokea maelezo kutoka kwa msimamizi wa mradi wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme wa JULIUS NYERERE MW 2115 Mhandisi Steven Manda jana April 5, 2020. Alipofanya ziara ya kukagua maendelelo ya mradi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...