Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
NAIBU
Waziri wa Afya, Dkt. Faustine Ndugulile amewashauri watu wenye magonjwa
sugu kuchukua tahadhari zaidi hasa kwa kupima afya na kufuata ushauri
wa wataalamu katika kukabiliana na ugonjwa unaosababishwa na virusi vya
Corona (Covid -19.) ambao hadi sasa maambukizi yake nchini yamefika
watu 32 na vifo vitatu.
Kupitia
ukurasa wake wa Twitter Ndugulile amechapisha taarifa iliyoeleza kuwa
mtu mwenye magonjwa sugu ikiwemo kisukari, shinikizo la damu, pumu,
ugonjwa wa moyo na unene uliopitiliza huathirika zaidi na Covid-19.
Aidha Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa mtu mwenye magonjwa hayo yupo kwenye hatari zaidi na wanaweza kupoteza maisha na
amewashauri
watu kuchukua tahadhari zaidi kwa kupima afya na kuzingatia ushauri wa
kitaalamu juu ya magonjwa hayo ili kupunguza madhara zaidi katika
kipindi hiki ambacho dunia inapambana katika kukabiliana na janga hilo.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya, leo Aprili 10, 2020
jumla ya watu walioambukizwa ugonjwa wa corona imefika 32, na
waliofariki dunia kutokana na ugonjwa huo imefikia watatu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...