Charles James, Michuzi TV

AFISA Tarafa wa Tarafa ya Itiso Wilaya ya Chamwino, Remedius Emmanuel amesema serikali ina nia njema ya kuwasaidia wakulima kupitia mfumo wa Stakabadhi ghalani kwenye zao la ufuta.

Remedius ameyasema hayo leo katika mkutano wake na wananchi wa Tarafa yake uliolenga kujenga uelewa wa pamoja na kutoa ufafanuzi juu ya azma ya Wakala wa Taifa was Hifadhi ya Chakula (NFRA) kuweka kituo cha kununulia mahindi katika Tarafa hiyo.

NFRA wameweka kituo hiko kwenye Kijiji cha Segala baada ya kuridhishwa na uzalishaji wa mahindi msimu huu wa kilimo ikiwa ni jitihada za Wilaya ya Chamwino kuhakikisha wakulima wanapata masoko yenye tija kwa mazao yao.

Katika juhudi za kutekeleza mpango huo, Remidius ameelekeza Maafisa Ugani wa Kata na vijiji kwa kushirikiana na Watendaji wa Kata na Vijiji kuwatambua wakulima wote wa zao la ufuta katika maeneo yao.

" Tunao mfumo wa Stakabadhi Ghalani kwa zao la ufuta, lakini Je katika maeneo yetu tunawatambua wakulima waliolima zao hili? Naomba kila kata na Kijiji tuwatambue wakulima hawa na kuandaa orodha itakayojumuisha majina yao, vitongoji vyao, hali ya uzalishaji na mawasiliano ya wakulima husika, hatua hii itasaidia sana kuwapatia taarifa sahihi kwa wakati kama sehemu ya mkakati wa kufanikisha mfumo huu kwa  Tarafa ya Itiso," Amesema Remedius.

Waakulima na wenyeviti wa vijiji  walioshiriki katika kikao hicho wamesema mpango huo wa Serikali ni mzuri  lakini zipo changamoto kadhaa  zinazohitaji kufanyiwa kazi kama njia muhimu ya kufanikisha adhma ya Serikali, huku wakitaja  kucheleweshwa  kwa Elimu (Uelewa) wa mfumo kwa wakulima wa zao la ufuta.

Kwa upande wake Afisa ushirika wa  Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Boniface Kobelo aliwataka  wakulima hao kuondoa shaka dhidi ya Mfumo wa Stakabadhi Ghalani na kwamba Changamoto zote zitashughulikiwa kwa wakati kwa  kwa kushirikiana na wadau wote katika mfumo huu.
 Wananchi na Wakulima katika Tarafa ya Itiso wakimsikiliza Afisa Tarafa wao, Remedius Emmanuel katika mkutano wa pamoja wa kujadili masuala mbalimbali ya kilimo.
 Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Boniface Kobelo akifafanua juu utaratibu unaotumika katika Mfumo wa Stakabadhi Ghalani pamoja na kujibu maswali yaliyoulizwa juu ya mfumo huo kwa zao la Ufuta.
 Baadhi ya Wakulima na Viongozi walioshiriki kikao hicho wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na   Afisa Tarafa pamoja na Ujumbe alioambatana nao.
 Afisa Tarafa ya Itiso, Remedius Emmanuel akizungumza na wananchi wa Tarafa yake katika mkutano wa pamoja wa kujenga uelewa juu ya zao la ufuta na azma ya NFRA kuweka kituo cha kununulia mahindi katika tarafa hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...