Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MAUAJI
ya Kimbari ya mwaka 1994 ambayo yanaelezwa kuwa ni mpango uliotekelezwa
na baadhi ya watu na kuuwa maelfu ya watu wa kabila la Watutsi nchini
Rwanda, mmoja ya watekelezaji wa tukio hilo Felician Kabuga
aliyekamatwa baada ya miaka 26 tangu kutokea kwa tukio hilo ameieleza
mahakama inayomshikilia nchini Ufaransa kuwa wampe dhamana wakati
akisubiri ni wapi kesi yake itasikilizwa aidha Ufaransa alipokamatwa au
nyumbani anakodaiwa kutekeleza mauaji hayo.
Felician
aliyekwepa mkono wa dola kwa miaka 26 anatuhumiwa kwa makosa 11 ikiwemo
kufadhili mpango wa utekelezaji wa mauaji ya Kimbari mpango uliogharimu
maisha ya watu zaidi ya milioni moja wa kabila la watutsi kwa siku 100,
Kabuga alifika mahakamani hapo akiwa katika kiti cha magurudumu na
kuiomba mahakama hiyo imuachie huru kwa kuwa afya yake si nzuri na ni
mzee ana miaka 87 huku nyaraka zote zikionesha ana umri wa miaka 84.
Aidha Kabuga ameieleza mahakama hiyo kuwa hakuhusika na mauaji ya mtusi yetote bali alikuwa anafanya nao kazi.
Kabuga
anadaiwa kufadhili silaha kwa watu wa jamii ya wahutu ambao
walitekeleza mauaji hayo ya mwaka 1994 na kutokomea kusikojulikana hadi
alipokuja kukamatwa mwaka huu nchini Ufaransa ambapo pia Marekani
iliweka dau la dola milioni tano kwa yeyote atakayetoa taarifa za wapi
alipo Kabuga.
Felician
Kabuga alikuwa mfanyabiashara maarufu akizalisha zao la chai nchini
Rwanda na alimiliki makampuni mengi yaliyotoa ajira nchini humo na nje
ya nchi, pia alimiliki kituo binafsi cha redio ambacho kinashutuhumiwa
kurusha habari zilizokuwa zikihamasisha wahutu kuwauwa watutsi.
Kabuga
ambaye alikuwa rafiki wa karibu wa kiongozi wa chama tawala Rais nchini
humo Juvenal Habyarimana ambaye ni mkwe wake aliyefariki mwaka 1994
anadaiwa kutumia utajiri na biashara kupanga na kufadhili mauaji hayo.
Kesi
hiyo imehairishwa hadi Juni tatu baada ya mahakama kutupilia mbali
maombi ya dhamana yaliyotolewa na Kabuga yakihusisha afya na uzee.
Felician
Kabuga amekana madai hayo ikiwa alikimbia nchini mwake na kujificha
huku akitumia majina ya uongo ili tu asikamatwe kwa miaka 26, je
ataachiwa huru? na ikiamuliwa kesi ikasomwe nchini mwake hisia za raia
wa Rwanda hasa watutsi itakuaje?
Kwa
ufupi Felician Kabuga alizaliwa Julai 9, 1935 huko Mukarange nchini
Rwanda, huku akiwa tajiri mkubwa na mfanyabiashara ambapo kabla ya
kutajwa kuhusika na tukio hilo mwaka 1995 alianzisha Kampuni ya biashara
nchini Kenya jambo ambalo aliyekuwa Rais wa Marekani Barack Obama
alipotembelea Kenya mwaka 2008 hakulibariki, kwa kuwa hata mpelelezi
nchini humo aliyejitokeza kusaidia kupatikana kwa Kabuga aliishia
kuuawa.
Mwaka 2020
jumamosi ya tarehe I6 Kabuga alikamatwa katika moja ya viunga huko Paris
Ufaransa na kuwekwa kwa muda katika gereza la La Sante'.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...