Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

WENGI hufikiri kuwa kuzaliwa kawaida ni kawaida, ila kwa Claudio Viera de Oliveira ni tofauti kabisa, yeye amezaliwa kichwa kikiwa kimeangalia juu pamoja na ulemavu wa mikono na miguu,na alipozaliwa madaktari walimshauri mama yake Maria Jose Vieira amuache Claudio afe kwani angemsumbua mno katika malezi lakini mama yake alipuuzia ushauri huo.

Licha ya ulemavu huo Claudio hakukata tamaa, akiwa na miaka 40 aliweza kuandika kitabu kilichohusu maisha yake kiitwacho  'Omundo Esta Ao Contrario:

Claudio raia wa Brazil alizaliwa na tatizo hilo ambalo hutokea mara chache sana, kitaalamu linajulikama kama 'arthrogryposis' hali ya misuli katika sehemu ya mwili kushindwa kujikunja na kujikunjua na kubaki ikiwa imekakamaa.

Claudio alianza kujifunza kuandika kwa kutumia mdomo ili aweze kupambana na changamoto iliyokuwa ikimkabili na aliweza kutimiza ndoto yake ya kuwa mhasibu pamoja na kutoa mihadhara katika matukio mbalimbali.

Akiwa na miaka 40 alichapisha kitabu chake cha kwanza kiitwacho  'Omundo Esta Ao Contrario' ambacho kimeelezea maisha yake  na uzoefu alioupata kupitia hali yake pamoja na mchango wa mama yake katika kufikia malengo.

Mama wa kijana huyo amewahi kueleza vyombo vya habari kuwa alishauriwa na madaktari kumwacha kijana wake afariki dunia kwa kuwa asingeweza kupumua vizuri na wengine walimshauri asimpe chakula lakini hakusikiliza ushauri huo.

"Alianza kutembea mwenyewe baada ya kubebwa kila mahali kwa miaka nane na alijifunza kufanya vitu kama watu wengine bila kuhitaji msaada, mwanangu anajiamini sana ninajivunia" alieleza mama huyo.

Claudio amenukuliwa akieleza kuwa tangu alipokuwa mtoto hakupenda kuwategemea watu wengine daima alikuwa akijishughulisha na kazi na amekuwa akijifunza kupitia televisheni, simu, redio pamoja na mitandao mbalimbali hadi akatimiza ndoto na kutunukiwa shahada ya uhasibu katika chuo kikuu cha Feira de Santana.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...