Na Zainab Nyamka, Michuzi TV

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA wamekabidhiwa bohari kuu ya maji,  miradi mikubwa 19, miradi midogo 322 kwa ajili ya kuanza kuihudumia.

Tukio hilo la uwekaji wa saini mikataba ya makabidhiano imefanyika leo katika Makao Makuu ya Mamlaka hiyo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa utiaji saini, Katibu Mkuu ww Wizara ya MajiProf Kitila Mkumbo amesema ana imani kubwa na DAWASA katika uendeshaji na watasimamia vizuri miradi hiyo watakayokabidhiwa kutoka Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).

Amesema, mbali na kukabidhiwa miradi hiyo ila Serikali kupitia Wizara ya maji imefanya maamuzi ya kuikabidhi bohari ya maji iliyopo Dar es Salaam ambapo awali ilikua ikitumiwa na serikali kabka ya kuwa na mamlaka za miji.

"Kwa sasa bohari hii itakuwa chini ya Dawasa, awali ilikua inatumika na serikali kununua vifaa na dawa ila toka kuanzishwa kwa Mamlaka za maji mijini wamekuwa wananunua wenyewe na kutokufanya kazi,"

Mkumbo amesema, Dawasa wanafanya kazi vizuri hata malalamiko yamepungua kwa kiasi kikubwa na kuna maeneo ambayo hayakuwa na huduma ya maji wamepata na changamoto imekwisha kwahiyo kukabidhiwa kwa miradi hiyo waende kufanya kazi.

Aidha, amesema jumuiya za maji 68 wanazokabidhiwa wakazitendee haki na miradi yote lazima watoe taarifa kwa Halmashauri zote za Wilaya na serikali za Mitaa  na kuweka uraratibu wa kupata taarifa kutoka kwa viongozi.

Mkumbo ameeleza wakandarasi wote wanaosimamia miradi iliyokabidhiwa kwa Dawasa walipwe madeni yao ma wakamilishe miradi kwa wakati uliopangwa ingawa ipo yenye muda mrefu nayo ikamilike ili wananchi wapate maji safi.

Kwa upande wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Mhandisi Cyprian Luhemeja amemuhakikishia Katibu Mkuu kuwa wapo tayari kusimamia miradi hiyo na watahakikisha inamalizika ili wananchi wanufaike kwa kunywa maji safi.

Luhemeja amewaomba wakandarasi kufanya kazi kulingana na mikataba yao inavyowataka kwani Dawasa hawataweza kuvumilia kuona miradi inachelewa kumalizika kwa wakati.

Kaimu Mkurugenzi wa RUWASA, Mkurugenzi wa Mipango na Uratibu Enock Wagala amesema wamekabidhi miradi hiyo kwa Dawasa ila wamekubaliana na serikali kuwa madeni yote zaidi ya Bilioni 2 wanazodai wakandarasi watalipwa ndani ya muda mfupi.

Hafla hiyo fupi ilimalizika kwa pande zote kuweka saini za makabidhiano ya miradi ya maji, bohari ya maji na kusaini mkataba wa kuhamisha mikataba ya wakandarasi kutoka Ruwasa kwenda Dawasa.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Prof Kitila Mkumbo pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhadisi Cyprian Luhemeja wakionesha mkataba wa makabidhiano  ya Bohari Kuu, hafla iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Prof Kitila Mkumbo  na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhadisi Cyprian Luhemeja wakikabidhiana mkataba wa makabidhiano  ya Bohari Kuu, hafla iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Prof Kitila Mkumbo  na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhadisi Cyprian Luhemeja wakisaini mkataba wa makabidhiano  ya Bohari Kuu, hafla iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhadisi Cyprian Luhemeja, Kaimu Mkurugenzi Ruwasa, Mkurugenzi wq Mipango na Uratibu Enock Wagala(kulia) sambamba na Moja ya wakandarasi wakisaini  mkataba wa makabidhiano  ya miradi ya maji na mikataba ya wakandarasi kwa Mamlaka ga Dawasa, hafla hiyo imefanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...