Charles James, Michuzi TV
KATIKA kuunga mkono mapambano dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Dk Ombeni Msuya amekabidhi mashine za kunawa wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro.

Dk Msuya amekabidhi mashine mbili katika Zahanati ya Mamba iliyopo Ugweno Mwanga pamoja na Mashine zingine mbili katika soko la Kikweni lililopo ndani ya Tarafa hiyo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Dk Msuya amewataka wananchi hao wa Mwanga kuendelea kuchukua tahadhari kama ambavyo serikali na watalaamu wake wamekua wakishauri ili kuweka kujikinga na Ugonjwa huo.

" Niwaombe ndugu zangu mzidi kuchukua hatua kwa kuvaa barakoa, kunawa mikono yenu kwa maji yanayotiririka pamoja na sabuni lakini pia kuwahi hospitalini mara tu unapohisi dalili za ugonjwa huu.

Ni jukumu letu sote sisi kama wananchi kushirikiana na serikali yetu katika kutoa elimu ya kujikinga na ugonjwa huu lakini pia kusaidia vifaa kama hivi ili kuweza kusaidia kujikinga na ugonjwa wa Corona, " Amesema Dk Msuya. 
 Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Dk Ombeni Msuya (wa kwanza kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wananchi wa Ugweno, Mwanga baada ya kuwagia mashine za kunawia ikiwa ni jitihada za kupambana na maambukizi ya Corona.
Wananchi mbalimbali wa Tarafa ya Ugweno wilayani Mwanga, Kilimanjaro wakinawa mikono kwa kutumia mashine za kisasa ambazo wamekabidhiwa leo na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) katika maeneo ya Zahanati na Soko.

Mhadhiri wa UDOM, Dk Ombeni Msuya akimuelekeza mmoja wa wananchi wa Tarafa ya Ugweno, Mwanga jinsi ya kutumia mashine za kunawia mikono mahususi kwa ajili ya kujikinga na Corona.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...