NA DENIS MLOWE,IRINGA

STENDI kuu ya Igumbilo na stendi ya zamani zimekabidhiwa msaada wa mashine ya kunawia mikono ya kisasa kutoka kwa kampuni ya Asas ya mjini Iringa ikiwa ni mwendelezo wa kampuni hiyo kusaidia jamii kupambana na kuenea kwa virusi vya coroni mkoani hapa.

Msaada huo wa mashine mbili za kisasa ambazo zinazinatumia miguu kuweza kutoa maji na vitakasa mikono ni kubwa zinazoweza kuhudumia watu zaidi ya watano kwa wakati mmoja zimekabidhiwa na mwakilishi wa kampuni hiyo, Afisa Usalama, Afya Mazingira na Ubora wa Kampuni ya Asas Cosmas Charles kwa niaba ya mkurugenzi wa uzalishaji wa kampuni hiyo, Ahmed Salim Abri kwa wenyeviti wa stendi hizo.

Cosmas alisema kuwa kutokana na wanafunzi wa vyuo na kidato cha sita wakitarajiwa kuendelea na masomo yao Juni 1 kampuni ya Asas Group imehimarisha huduma ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kwa abiria wanaotumia stendi kuu za mjini Iringa kuongeza mashine za kisasa za kunawia mikono kwa lengo la kuhudumia wananchi wengi zaidi.

Alisema kuwa kampuni imetoa mashine hizo zenye uwezo wa kuhudumia watu sita kwa mara moja kwa kila moja zimetolewa katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani ya Igumbilo, mjini Iringa na stendi kuu ya daladala zinazotoa huduma katika maeneo mbalimbali ya mjini huo.

“ Kama kampuni tumelenga maeneo yenye mikusanyiko mikubwa, tukianzia na stendi kuu za mjini Iringa na baadae tutaenda kwenye maeneo mengine ambayo pia yana mikusanyiko mikubwa ya watu ndani na nje ya mkoa kwa lengo la kusaidia jamii kuweza kupambana na maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa Covid 19,” alisema.

Aidha alisema kuwa kampuni hiyo imekwishatoa msaada wa ndoo maalumu za kunawia mikono, barakoa na vitakasa mikono kwa makundi mbalimbali ya jamii mjini Iringa, wakiwemo madereva wa daladala, bajaji na bodaboda.

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Mwenyikiti wa Stendi ya Igumbilo, Mwinyi Mwaugali alisema kuwa wanakumbana na changamoto kubwa ya uhaba wa vifaa vya kunawihia kwenye stendi hiyo kutokana na kuwa kubwa hivyo msaada huo umekuwa muhimu sana kwa wanaotumia stendi hiyo.

Mwaugali aliishukuru kampuni ya Asas na kutoa wito kwa kampuni ya hiyo kuangalia uwezekano wa kuongeza mashine zingine kama hii kwasababu katika stendi hii kuna maeneo saba ya kushusha na kupakia abiria hivyo zitasaidia kwa kiasi kikubwa

Kwa upande wake askari wa usalama barabara wa kituo kikuu cha daladala cha mjini Iringa, Koplo Rashid aliwataka abiria na watu wengine wanaotumia kituo hicho cha daladala kuitumia mashine hiyo ili kujinusuru na janga hilo.

“Asas ametoa msaada huu kwasababu anawapenda watu, ombi langu kwa watu wote wanaotumia stendi hii tusiigeuze mashine hii kuwa pambo, ifanye kazi iliyokusudiwa ili kutunusuru na maambukizi ya virusi hivyo,” alisema.

Mmoja wa wapiga debe kwenye stendi kuu ya Igumbilo akifurahia msaada wa mtambo wa kisasa wa kunawia mikono uliotolewa na kampuni ya Asas kwa ajili ya abiria na wafanyabiashara kwenye stendi hiyo unaoweza hudumia watu zaidi ya watano kwa wakati mmoja.
Afisa Usalama, Afya Mazingira na Ubora wa Kampuni ya Asas Cosmas Charles akitoa elimu jinsi ya kutumia mashine hiyo kwa baadhi ya wananchi wanaotumia stendi hiyo kwa shughuli za kila siku.(picha na Denis Mlowe)
Abiria na wananchi wakinawa mikono mara baada ya kupatiwa msaada wa mashine kutoka kampuni ya Asas (picha na Denis Mlowe).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...