Na Leandra Gabriel, Michuzi TV


KIM Jong - un kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini "Master" anafahamika zaidi kwa uongozi wake wa kidikteta pamoja na kutoweka wazi baadhi ya masuala yanayomuhusu, ikiwemo umri, familia hasa idadi ya watoto na safari yake kielimu, Kim amezaliwa Korea Kaskazini ni kijana wa bi.Young -hee na bwana Kim Jong -il aliyetawala nchi hiyo kidikteta hadi alipofariki dunia mwaka 2011.


Kim Rais wa Korea Kaskazini na kiongozi wa chama cha wafanyakazi wa nchi hiyo ni mtoto wa pili Kim Jong -il (1941-2011,) kabla ya kupewa madaraka hayo na kabla ya kufariki kwa baba yake Jong -il Kim hakuwa anaonekana mara kwa mara kwa umma ndio maana maelezo ya kusoma Uswisi na kutumia majina ya uongo ni ngumu kuthibitisha.


Mwaka 2009 taarifa zilianza kuenea kuhusiana na uteuzi wa Kim kumrithi baba yake aliyekuwa mgonjwa ambapo alipewa nafasi katika jeshi ambako nyimbo kusifu familia ya Kim zilitungwa, mwaka 2010 alipewa nafasi ya ujenerali jeshini kabla ya kutangazwa rasmi kuwa mrithi wa baba yake baada ya mazishi Desemba 28 mwaka 2011, na amebahatika kuwa na mke na watoto wawili Ju Ae na wengine wawili walioripotiwa.


Licha ya kusimamia vyema sekta za kilimo na uchumi, uvunjifu wa haki za binadamu bado unaripotiwa nchini humo, na hiyo ni pamoja na kuendeleza kutumia nguvu za nyuklia jambo ambalo lilipangwa kusitishwa ambapo Kim alikutana na Rais wa Korea Kusini Moon Jae -in na Rais wa Marekani Donald Trump mwaka 2018 ili kuweka makubaliano mbalimbali ikiwemo kusitisha matumizi ya nguvu za nyuklia jambo ambalo halijaanza kutekelezwa.


Yanayomuhusu Kim Jong -un maarufu kama Master ni pamoja na haya;


Anaweza kuwa kiongozi mdogo zaidi wa ulimwengu, lakini hakuna mtu mwenye uhakika na umri wake halisi, maandiko na watu wanaeleza kuwa alizaliwa mnamo Januari nane mwaka1982, 1983 au 1984.


Kuanzia mwaka 2002 hadi 2007 Kim alipata shahada mbili alizozipata katika chuo kikuu cha kijeshi cha Kim II-sung ambako alitunukiwa shahada za Fizikia na ile ya masuala ya kijeshi.Aliwahi kufanyiwa upasuaji kwa madai ya kutaka kufanana na babu yake Kim Il Sung na mwaka 2012 jarida moja nchini humo lilimtangaza kuwa mwanaume mwenye mvuto zaidi.


Baada ya baba yake kufariki dunia alihakikisha kifo chake kinaombolezwa kwa moyo na Wakorea wa Kaskazini wote na wale ambao hawakwenda kwenye hafla za kuomboleza waliripotiwa na kuhukumiwa kwenda katika kambi za kazi kwa miezi sita.


Vilevile katika kumbukizi ya kifo cha babu yake Kim il Sung, na baba yake Jong il alihakikisha kuwa nchi yote inaomboleza.


Licha ya kuongoza kidikteta, kutokuwa na uchaguzi wa huru na haki, wanahabari kutokuwa na uhuru pamoja na kutokuwa na uhuru wa dini Kim anaelezwa kuwa ametekeleza vifo ya watu wengi, ikiwemo cha kaka yake wa kambo Kim Jong -nam (2017) aliyeuwawa kwa kupewa sumu katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur nchini Malysia na wachunguzi kueleza kuwa Kim alitekeleza hilo na hiyo ni pamoja na watu wengi kuishia jela bila sababu pamoja na kutoa adhabu kwa familia nzima hata kosa likitendwa na mtu mmoja.

Licha ya kuonesha tabasamu kila wakati Kim anaelezwa kuwa ni mtu msiri mno; hajawahi weka picha ya utoto hadharani, licha ya picha yake ya utoto kuwekwa hadharani mwaka 2014 katika sikukuu ya majeshi ikiwa ni picha ya kiongozi akiwa mtoto na hakuna aliyefahamu kuwa ni yeye.

Kuhusu elimu yake, Inaelezwa kuwa alisoma nchini Uswis kwa majina tofauti ambayo ni Chol-pak au Pak -Chol katika miaka ya 1998 na 2000 ambapo imeelezwa kulikuwa na wanafunzi kutoka Korea Kaskazini chuoni humo, na licha ya kujisajili kupitia ubalozi baadhi ya wanafunzi aliosoma nao wanaamini ni yeye huku wengi wakieleza alikuwa na vituko na aliyependa michezo na hakuwa mwanafunzi bora sana darasani.

Kwa mwaka 2020 mujibu wa Shirika la utangazaji la kimataifa la Al-jazeera imeelezwa kuwa mwaka huu Kim hajatokea hadharani kama ilivyokuwa awali, tokea mwanzoni mwa mwezi Aprili hadi Mei ameonekana mara nne pekee ukilinganisha na mara 27 alizoonekana katika kipindi hicho kwa mwaka uliopita.

Wachambuzi wa mambo wameeleza kuwa huenda ikawa ni sehemu ya kupambana na mlipuko wa virusi vya Corona ambapo hadi sasa nchi hiyo haijaripoti kisa chochote huku tetesi za kiongozi huyo kuugua hadi kushindwa kuhudhuria sherehe kuu ya nchi hiyo zikielezwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...