Baada ya Bundesliga kuanza kutimua vumbi, Pazia la ligi Kuu nchini Uingereza linatarajia kufunguliwa Juni 17 mwaka huu kwa mechi mbili kuchezwa.

Mechi hizo zikiwa ni viporo zitawakutanisha mabingwa watetezi Manchester City dhidi ya Arsenal na Aston Villa dhidi ya Sheffield United huku ratiba kamili ikianzia wikiendi ya Juni 19-21.

Bado kuna jumla ya mechi 92 ambazo zinahitaji kuchezwa na vilabu vyote 20 baada ya Ligi hiyo kusiimamishwa kwa muda usiojulikana Machi 13 kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

Inatimia siku 100 toka Ligi hiyo kusimama mechi ya mwisho ikiwa ni Leicester City dhidi ya Aston Villa wakishinda 4-0 na itarejea bila kuwa na mashabiki uwanjani.Kwa sasa klabu zote zimekubaliana kuanza mazoezi ya wachezaji kwa kugusana ikiwa ni hatua ya pili baada ya mazoezi binafsi kuanza toka juma lililopita.

Watu 2,752 wanaohusika moja kwa moja na Ligi hiyo walipimwa na Kufikia leo watu 12 (wakiwemo wachezaji na maafisa wa timu) wamekutwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

Bodi ya Ligi imesisitiza kuwa wachezaji na maafisa wataendelea kupimwa mara mbili kwa wiki na Wale watakaoqkutwa na maambukizi watatakiwa kujitenga na wenzao kwa muda wa siku saba.

Mipango inayofuata kwa sasa ni kuidhinisha mazoezi ya pamoja na kawaida kwa klabu kujifua na michezo ya ushindani.Klabu ya Liverpool ipo kileleni mwa ligi hiyo kwa utofauti wa alama 25 huku ihitaji kushinda mchezo mmoja tu ili kutawazwa kuwa mabingwa.

Kwa upande wa pili wa shilingi, klabu za Bournemouth, Aston Villa na Norwich City zipo mkiani na katika hatari ya kushuka daraja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...