Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi,  leo hii amekabidhi vifaa maalumu vya kujikinga na virusi vya Corona usoni (Face Shields) vipatavyo 150 kwa hospitali na vituo vya afya 22 katika Manispaa za mkoa wa Dar es Salaam.

Lengo la CCBRT ni kuunga mkono juhudi za Serikali na wadau wengine hapa nchini katika kuwakinga wahudumu wa afya na janga la Corona. 

“Tumekusudia vifaa hivi vitumike katika vitengo vya afya ya uzazi katika hospitali hizo ili kuwakinga wahudumu wa afya ambao kila siku wamekuwa mstari wa mbele kuokoa maisha ya mama na mtoto”, amesema Mkurugenzi huyo wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo kwa wawakilishi wa hospitali hizo kutoka Manisapaa 5 za mkoa wa Dar es Salaam.

 Aliendelea kusema kuwa vifaa hivi vitasaidia kuwaweka salama watoa huduma salama wakati wakiwahudumia wagonjwa.

Kwa takribani kipindi cha miaka 10, CCBRT kwa kushirikiana na Timu ya Afya ya Mkoa wa Dar es Salaam (RHMT) na Timu za Afya za Manispaa (CHMTs), wamekuwa wakiendesha mradi wa kujenga uwezo wa watumishi wa afya eneo la afya ya  uzazi katika hospitali,vituo vya afya na zahanati 22 katika Manispaa zote tano za Mkoa wa Dar es Salaam. 

Kwa sasa mradi huu pia unafanya kazi na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Mloganzila hasa kwenye upande wa rufaa za wagonjwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...